Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mpina ataka uchunguzi Symbion kabla ya kulipwa
Habari za Siasa

Mpina ataka uchunguzi Symbion kabla ya kulipwa

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina
Spread the love

 

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, ameishauri Serikali ifanye uchunguzi dhidi ya Kampuni ya kuzalisha umeme ya Symbion Power, kabla ya kuilipa zaidi ya Sh. 356 bilioni kufuatia hatua yake ya kuvunja mkataba kati ya kampuni hiyo na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mpina ametoa ushauri huo leo Jumatatu, tarehe 9 Mei 2022, akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Uwekezaji kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, bungeni jijini Dodoma.

Ushauri huo wa Mpina umetolewa baada ya ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha wa 2020/21, kubaini Serikali imetakiwa kulipwa mabilioni hayo ya fedha baada ya kuamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC), nchini Uingereza.

“Sasa hivi nasikia Symbion inapigiwa chapuo tuilipe Sh. 356 bilioni, lakini chapuo hili linapigwa wakati hatuambiwi aliyeingia mkataba huo na kusababishia tuwe na mkataba huo ambao hatuwezi kuumudu unatuingizia hasara amechukuliwa hatua gani?” amesema Mpina.

Mpina amesema “hatuambiwi kwamba huyu Symbion malimbikizo yake ya kodi ni shilingi ngapi na anapaswa kutulipa shilingi ngapi, linapigwa chapuo hatuambiwi ukaguzi gani umefanyika juu ya mambo yaliyojificha nyuma ya pazia hili. Tukatae kulipa hizi fedha, ukaguzi wa kina ufanyike ili tuweze kuyajua yote.”

Mpina ameshauri mikataba mibovu ya uwekezaji ambayo taasisi za Serikali imeingia na sekta binafsi, ipelekwe bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo ametaka uchunguzi ufanyike katika Bodi ya Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ili kujua ukweli kuhusu tuhuma za kuwepo ufisadi unaosababisha bei ya mafuta kuwa juu.

Mpina amesema sasa hivi kisingizio kimekuwa ni tozo na kupuuza tuhuma ambazo zimeelezwa kungeni kuhusu uwepo wa kasoro katika tenda za uagizaji mafuta.

Itakumbukwa hivi karibuni Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu aliomba Bunge liahirishwe ili kujadili tuhuma za tenda za uagizaji mafuta kuchezewa.

Hata hivyo Spika Tulia Akson alimkatisha kutoa hoja hiyo na kusema jambo hilo ni zito hivyo litahitaji Ushahidi na kwamba litaibua mambo mengi zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!