Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge aitaka Serikali iunde kikosi kazi cha uchumi
Habari za Siasa

Mbunge aitaka Serikali iunde kikosi kazi cha uchumi

Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi
Spread the love

 

MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi, ameitaka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuunda kikosi kazi cha masuala ya uchuimi kama ambayo imeunda kikosi kazi cha masuala ya siasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Ameyasema hayo leo Jumatatu tarehe 9 Mei 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hoja ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Chumi amesema lazima taifa likubaliane kuwa kuna mambo ya kukataa ikiwemo kuagiza bidhaa ambazo zinawezekana kuzalishwa hapa nchini akitolea mfano, sukari, ngano na mafuta ya kula.

Mbunge huyo ameonesha kutofurahishwa na uagizaji wa kila kitu kutoka nje na kusema, “kitu ambacho hatuagizi ni hewa tu ya Mwenyezi Mungu ambayo ametujalia.”

Amesema ameshaandika barua kwa mawaziri wa sekta za uzalishaji na kuishauri Serikali kuweka mikakati ya kuzalisha sukari ya kutosha hapa nchini na kuachana na uagizaji kutoka nje.

Alitoa mfano wa Brazil ambao ni wazlishaji wakubwa wa sukari duniani kuwa wanatumia uzalishaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo havihitaji mtaji mkubwa kuwekeza.

Mbunge huyo amesema viwanda hivyo vinagharimu kati ya Dola za Marekani milioni 3.5 hadi 5 sawa na shilingi bilioni nane za kitanzania.

Ameshauri Halmashauri kutenga maeneo kwaajili ya kilimo na Serikali kupitia benki ya kilimo kuwezesha upatikanaji wa mitaji na wiraza kuwezesha miundombinu mingine kitakayohitajika katika uzalishaji huo.

“Kama Rais ameunda kikosi kazi kwaajili ya kutafuta mazingira mazuri ya ufanyaji siasa kwanini sasa Waziri asiunde ‘kitchen cabinet’ kikosi kazi cha uchumi?” alihoji Chumi.

Amemtaka Waziri kuchukua wataalam kutoka taasisi za elimu ya juu ili kuunda kikosi kazi kiweze kusahauri kuhusu uzalishaji nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!