Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nchemba, Shigongo wavutana nchi kurudi uchumi wa chini
Habari za SiasaTangulizi

Nchemba, Shigongo wavutana nchi kurudi uchumi wa chini

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo
Spread the love

 

MVUTANO umeibuka bungeni baina ya Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba kuhusu nchi kuporomoka kutoka uchumi wa kati hadi uchumi wa chini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mvutano huo umeibuka leo Jumatatu tarehe 9 Mei 2022 baada ya Shigongo kueleza bungeni hapo kuwa taifa limeporomoka kutoka uchumi wa kati hadi uchumi wa chini tofauti na miaka miwili iliyopita.

Mbunge huyo amesema pato la mtu mmoja mmoja limeshuka hadi Dola za Marekani 976 na hivyo kuifanya Tanzania kukosa sifa zinazoifanya nchi kuwa uchumi wa kati.

“Nchi yetu Tanzania miaka miwili iliyopita tulisheherekea tukashangilia kwa pamoja kupanda mpaka uchumi wa kati, GDP ya Taifa ilikuwa, per capita income ikaongezeka na hivyo tukasheherekea kwamba nchi yetu inakwenda vizuri.

“Lakini ninavyozungumza na wewe hivi sasa nchi yetu imerudi tulipokuwa, ‘per capita income’ imeshuka hadi dola 976, ina maana tumeporomoka chini kwasababu yeyote ile iwe covid au yeyote ile ukweli tumeporomoka,” amesema.

Wakati akieleza hayo Dk. Nchemba aliomba kuweka sawa jambo hilo na kueleza kuwa kilichoshuka ni ukuaji wa uchumi (growth rate)na si viwango vya pato la Taifa (level of income).

“Nataka niweke kumbukumbu sawa kwamba hatujarudi tulipokuwa na hii naomba isikike vizuri sana. Tulitoka uchumi wa chini tukaenda uchumi wa kati wa chini hatujawahi kurudi uchumi wa chini tena,” amesema Nchemba.

Ameongeza, “tunachozungumza ni ukuaji na si level ya uchumi. Kuna tofauti ya level of income ya nchi na growth rate.”

Amesema kilichobadilika ni kutoka ukuaji wa asilimia saba na kushuka hadi asilimia nne ya ukuaji wa uchumi “na tangu tushuke tushapanda hadi 4.9.”

Waziri huyo amesema kwa takwimu zinazokamilika za 2021 ukijumlisha wastani wanaenda asilimia tano “na kwa mwaka 2022 tunaenda asilimia 5.2 na hata wenzetu wa Benki ya dunia juzi walisema huenda tukaenda hata 5.5.”

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Hata hivyo Shigongo hakukubaliana na hoja za Nchemba ambapo alieleza kuwa kigezo kinachotumika nchi kuwa uchumi wa kati ni kuwa na pato la mtu mmoja mmoja la kati ya Dola za Marekani 3033 hadi 4045 na kwamba Tanznaia ilifikia Dola 3080 ndiyo ikafika uchumi wa kati.

Alisema kwa takwimu za sasa pato la mtu mmoja mmoja limefikia Dola za Marekani 976 hivyo ni Dhahiri kuwa nchi imerudi uchumi wa chini.

“Ndiyo maana na sema tumerudi kwasababu ‘per capita’ imeshuka, hoja yangu ni kwamba kurudi nyuma sio sababu cha msingi ni kushirikiana na wabunge turudi tulikokuwa uchumi wa kati, na hili litawezekana kwa kuimarisha kilimo kwa kutafuta masoko.,” amesema Shigongo.

Shigongo ameomba TANTRADE kupewa fedha za kutosha ili iweze kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo za Tanzania badala ya kuishia kuandaa maonesho ya sabasaba.

1 Comment

  • Mama unashauruwa vibaya!
    Kazi ipo. Ni pato la mtu na si ukuaji wa uchumi.
    Pia, tumieni maendeleo ya uchumi na si ukuaji wa uchumi peke yake. Hatuna teknolojia ya kutosha kusimamia ukuaji wa uchumi.
    Kwa hiyo, serikali ilikuwa na fedha za kutosha miaka Ile na sasa wamechota wale wezi, hazina, benki kuu na kwingineko. Ndiyo, tumerudi kwenye umaskini kwa sababu ya uizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!