Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Biashara madini nchini yaimarika bei ikipaa
Habari za Siasa

Biashara madini nchini yaimarika bei ikipaa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) akiangalia madini ya Tanzanite kwenye kampuni ya Tanzanite Forever Lapidary (T) LTD inayomilikiwa na Faisal Juma Shabhai (kulia) alipotembelea Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Spread the love

 

WAZIRI wa Madini, Doto Biteko, amesema biashara ya madini nchini imeendelea kuimarika huku bei ya madini muhimu kama dhahabu na almasi ikizidi kuongezeka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Biteko ameyasema hayo bungeni leo Ijumaa tarehe 29, Aprili, 2022 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi yam waka 2022/2023.

Waziri huyo amesema katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi 2022 zimezalishwa jumla ya kilogramu 39,682.94 za dhahabu, kilogramu 7,102.96 za fedha, karati 155,117.10 za almasi.

Pia zimezalishwa kilogramu 15,377.44 za Tanzanite ghafi, kilogramu 130,582.28 za Tanzanite za ubora wa chini (beads), karati 81,305.42 za tanzanite iliyokatwa na kusanifiwa, tani 19,355.13 za madini ya shaba na tani 322.4 za madini ya bati.

Mbali na madini hayo Biteko amesema pia zimezalishwa, kilogramu 6,835,746.73 na karati 12,863.29 za madini mengine ya vito ghafi na vito vilivyokatwa na kusanifiwa mtawalia, tani 18,462,591.96 za madini ya ujenzi.

Aidha zimezalishwa tani 956,688.08 za makaa ya mawe, tani 7,843,634.41 za madini mengine ya viwandani, na tani 51,132.33 za madini mengine ya metali zilizalishwa na kuuzwa.

Kutokana na uzalishaji huo Biteko amesema katika kipindi hicho shilingi 429 bilioni zilikusanywa kama malipo ya mrabaha na ada ya ukaguzi kutoka kwenye madini hayo yenye thamani ya shilingi 6.4 trilioni.

Amesema makusanyo hayo ni ongezeko la asilimia 2.5 ikilinganishwa na shilingi 418.7 bilioni zilizokusanywa katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2020/2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!