Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polepole aanza safari ya Malawi
Habari za Siasa

Polepole aanza safari ya Malawi

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amemweleza Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole umuhimu wa kuifanyia kazi na kuipa kipaumbele Sera ya Diplomasia ya Uchumi nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Rais Mwinyi alisema hayo jana Alhamisi, tarehe 29 Aprili 2022, alipozungumza na Balozi huyo, aliyefika Ikulu mjini hapa kuaga akiwa tayari kwenda kwenye kituo chake kipya cha kazi nchini humo.

Katika mazungumzo hayo, Rais Mwinyi alimweleza Balozi Polepole kwamba Tanzania imeelekeza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi na nchi za nje, ambayo ndiyo dira yake katika ushirikiano na nchi hizo kiuchumi.

Hivyo, alisisitiza haja kwa kiongozi huyo kuifanyia kazi Sera hiyo, hasa katika sekta ya biashara.

Kwa Zanzibar, Rais Mwinyi alimweleza Balozi Polepole kwamba ina mazao mengi yanayotokana na bahari ambayo ni bidhaa muhimu katika biashara nje ya nchi, wakiwamo dagaa ambao bado hawajapata soko Malawi.

Aliongeza, kwa hivi sasa biashara ya dagaa kutoka Zanzibar imekuwa ikifanyika zaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuimarika kwa kiasi kikubwa, hivyo ni vema fursa hiyo ya kibiashara ikatumika Malawi.

Aidha, Rais Mwinyi alieleza, kwamba mbali na suala la kiuchumi na kibiashara,Tanzania ilishiriki vema kupigania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika ikiwamo Malawi, hivyo ni vema uhusiano na ushirikiano wa kimipaka ukaendelezwa hasa kwa vile nchi hizo zinapakana.

Alisisitiza, kwamba ushirikiano wa mipaka ukiimarika, utasaidia kupambana na kukinga vitendo viovu vya kiulinzi na kiusalama na kulinda mipaka kati ya nchi mbili hizo.

Sambamba na hayo, Rais Mwinyi alimpongeza Balozi Polepole kwa kuteuliwa na kumhakikishia, kwamba Serikali ya Zanzibar itampa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza jukumu lake hilo jipya.

Balozi Polepole alimhakikishia Rais Mwinyi, kuyafanyia kazi maelekezo aliyompa, kwa kutambua kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.

Alisema kwa vile Zanzibar imejikita kuweka mikakati ya kuimarisha uchumi wa buluu, atahakikisha Sera hiyo anaifanyia kazi kwa kutafuta fursa hasa za biashara zinazotokana na rasilimali za bahari, ikiwamo bidhaa ya dagaa katika soko la Malawi.

Pamoja na hayo, Balozi Polepole alimpongeza Rais Mwinyi kwa kuendeleza na kukuza uchumi wa Zanzibar, hasa katika sera ya uchumi wa buluu ambayo aliahidi kwenda kuifanyia kazi Malawi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!