Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko SAG wafuturisha watoto yatima Mtambani
Habari Mchanganyiko

SAG wafuturisha watoto yatima Mtambani

Mmoja wa watoto yatima wanaolelewa na Msikiti wa Mtambani, Lawwal Mohammed (katikati) akiomba dua kushukuru wafanyakazi wa Kampuni ya Smart Africa Group (SAG), baada ya kukabidhiwa msaada wa vyakula. Kushoto ni Imam wa Msikiti wa Mtambani, Suleiman Abdallah na Ofisa wa SAG, Nawadh James.
Spread the love

 

KAMPUNI za Smart Africa Group (SAG) imetoa msaada wa vyakula na mafuta kwa ajili ya futari kwa watoto yatima wanaosoma kwenye shule ya msingi ya Mtambani. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Msaada huo umetolewa leo tarehe 26 Aprili 2022 na kampuni hizi zilizokuwa chini ya mwamvuli wa SAG, kwa lengo la kuwafariji watoto hao.

SAG inajumuisha wa kampuni tano ambazo ni pamoja na Smart Codes, Smart Lab, Smart Studio, Smart Nology na Smart Foundry.

Akizungumza kwa niaba ya Kampuni hizo,  Emmanuel Kawedi amesema wamewiwa kutoa msaada huo ili kuwasaidia watoto yatima kwa kuwa hawana nguzo zao muhimu za kimalezi.

Kawedi amesema Kampuni hiyo imekabidhi vyakula, mafuta, kwa ajili ya futari na chakula chab watoto hao.

Sheikh Suleiman Abdallah ambaye ni Imam wa Msikiti wa Mtambani na Mlezi wa shule ya Msingi Mtambani na Sekondari Mvumoni ameishukuru SAG kwa kuwakumbuka watoto yatima waliokuwepo kwenye shule hiyo.

Ameeleza kuwa shule hiyo iliyokuwa chini ya Msikiti wa Mtambani ina wanafunzi 300 ambapo wanafunzi 50 ni yatima na ndio waliolengwa kwenye msaada huo.

Amesema kuwasaidia watoto yatima kunapelekea maisha ya mtoaji kuwa na Baraka.

“Niwape siri moja… kuwasaidia watoto yatima kunaongeza baraka kwenye maisha Mwenyezi Mungu humuondolea matatizo mtu anayewasaidia watoto yatima” amesema Sheikh Abdallah.

Amesema wanafunzi hao yatima wanasomeshwa kwa sadaka za waumini wanaoswali kwenye msikiti wa mtambani.

Sheikh Abdallah amesema Mkurugenzi Mtendaji wa SAG, Edwin Bruno ameonesha nia ya kusaidia kuwalipia ada wanafunzi hao.

Kampuni hizo zimejikita kwenye mapinduzi ya Kiteknolojia ambayo yameleta matokeo chanya nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!