May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maandalizi ya sensa yafikia asilimia 81

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Kamati Kuu ya Sensa ya Watu na Makazi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema maandalizi ya zoezi hilo hadi kufikia jana Jumatatu, tarehe 25 Aprili 2022, yamefikia asilimia 81. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Majaliwa ametoa taarifa hiyo leo Jumanne, katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yaliyofanyika jijini Dodoma.

Amewataka wananchi wajitokeze kushiriki sensa inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti mwaka huu nchi nzima.

“Tarehe 23 Agosti 2022, itafanyika sensa ya watu na makazi ambao maandalizi yake yanaendelea vizuri. Kufikia jana jioni tulishafika asilimia 81 ya maandalizi,” amesema Waziri Majaliwa na kuongeza:

“Kwa lugha nyingine tunasema kwamba, kukataa kuhesabiwa ni kujinyima fungu lako katika mipango ya kitaifa kwani sensa ni kwa maendeleo ya taifa hili. Nitoe wito kufanya maandalizi ya kujitokeza sku hiyo na kupokea watalaamu wetu kwa ajili ya kuhesabiwa.”

error: Content is protected !!