Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Afrika Kusini yamshutumu Balozi wa Ukraine
Habari Mchanganyiko

Afrika Kusini yamshutumu Balozi wa Ukraine

Spread the love

AFRIKA Kusini imemshutumu Balozi wa Ukraine nchini humo, Liubov Abravitova kwa kutumia njia zisizo za kidiplomasia kuomba mazungumzo na Rais Cyril Ramaphosa.

Hayo yanajiri wakati Urusi ikiendelea kuishambulia Ukraine tangu ilipoanzisha mashambulizi tarehe 24 Februari, mwaka huu. Anaripoti Rhoda Kanuti… (endelea).

Balozi huyo alilazimika kutumia mtandao wa Twitter kuomba kukutana na Rais huyo.

Aidha, Balozi Abravitova ameishutumu mamlaka ya Afrika Kusini kwa madai ya kupuuza maombi yake mengi ya kukutana Ramaphosa pamoja na mawaziri wengine.

Amesema tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi hajapokea ombi lolote la mkutano kutoka kwa maofisa wa serikali ya Afrika Kusini.

“Watu wangu wanakabiliwa na mashambulizi ya kikatili kutoka kwa Warusi,” aliandika kwenye mtandao huo tarehe 10 Aprili, 2022 .

Aidha, Ofisa mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini, Clayson Momyela amekanusha madai hayo ya mjumbe huyo akisema kwamba tayari alikuwa ameishafanya mikutano na maofisa kadhaa wa serikali.

Balozi huyo alitetea hatua yake akisema kwamba “sina chaguo linguine maana watu wangu wanakufa, wanateseka, wanabakwa.”

Afrika Kusini inakabiliwa na ukosaji wa msimamo wa kutoegemea upande wowote, kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Wiki iliyopita nchi hiyo, ilijiepusha na kura ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, iliyotaka kuisimamisha Urusi katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!