Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili avigeuzia kibao vyama vya siasa madai ya demokrasia
Habari za Siasa

Msajili avigeuzia kibao vyama vya siasa madai ya demokrasia

Spread the love

NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amevitaka vyama vya siasa kuimarisha kwanza demokrasia ya ndani, kabla ya kutoka nje. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Nyahoza ametoa wito huo leo Jumanne, tarehe 5 Aprili 2022, akizungumza katika kongamano la haki, amani na maridhiano, lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na kufanyika jijini Dodoma.

“Kwa uzoefu wetu ambao tunakuwa na vyama tunavihakiki, tumeona kwamba katika vyama vya siasa bado lile suala la demokrasia havijajikita vizuri, vinajikita sana kuongelea demokrasia ya nje ya vyama kuliko ndani ya vyama. Na hapa nimeshaeleza malezi yanaanzia nyumbani,” amesema Nyahoza.

Nyahoza amesema “sisi tunahimiza vyama pia viangalie suala la demokrasia ndani ya vyama. Hata suala la maridhiano pia yaanzie ndani kwa sababu kule pia kuna masuala ya mtifuano ndani ya vyama.”

Naibu Msajili huyo wa vyama amesema, kuna baadhi ya vyama maridhiano na demokrasia hupotea, kinapofika kipindi cha uteuzi wa viongozi.

“Ndani ya vyama wakati wa uteuzi wa wagombea, wakati wa kutafuta viongozi wa vyama, nasikia kuna baadhi ukisema mimi mwenyekiti , ukisema una nia ya kugombea uenyekiti kesho kinaitishwa kikao cha kukufukuza.. Haya masuala lazima yajengwe kuanzia ndani ya vyama,” amesema Nyahoza.

Aidha, Nyahoza amesema ofisi yake inaendelea kuratibu kwa karibu shughuli za vyama vya siasa, ili zitekelezwe kwa mujibu wa sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!