WAKATI Serikali ikiendelea kuboresha huduma za elimu na afya maeneo mbalimbali nchini, ujenzi wa kituo cha Afya Narung’ombe wilayani Ruangwa mkoani Lindi umetajwa kumnufaisha mama lishe ambaye amenuia kununua kiwanja kwa kupitia biashara hiyo.
Mama Lishe huyo Shania Makota mwenye umri wa miaka 23, anawahudumia chakula mafundi ujenzi wanaojenga kituo hicho cha afya kilichopo katika kata ya Narung’ombe mkoani Lindi. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Makota amesema mbali na ndoto hiyo, sasa anawasomesha wadogo zake watatu na kuhudumia familia kwa kutumia kipato anachovuna kutokana na mradi huo,
“Wanaenda shule kupitia pesa ambayo naitafuta kwenye hii kazi, isingekuwa mradi huu sijui tungeishije… lakini ni dhahiri umetusaidia kwa sababu kupitia mradi huu nimepata pesa ya kuhudumia familia yangu, mama yangu pamoja na ndugu zangu.
“Huwa nawanunulia nguo, viatu, kiujumla mahitaji yote nawahudumia mimi. Mpaka kukamilika kwa mradi huu nitakuwa nimetimiza malengo yangu kadhaa kimaisha.
“Mpaka mradi ukamilike nimepanga ninunue kiwanja kupitia pesa nitakayoendelea kupitia kwenye huu mradi, Namshukuru sana Rais Samia, asiishie hapa aendelee na moyo huohuo,” amesema.
Leave a comment