Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Bei petroli yafika 3,105 kwa lita
Habari Mchanganyiko

Bei petroli yafika 3,105 kwa lita

Spread the love

BEI za nishati ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa nchini imeongezeka kwa asilimia 11 hadi 21 kuanzia leo Jumatano tarehe 6 Aprili 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Bei hizo mpya zimetangazwa jana Jumanne tarehe 5 Aprili 2022 na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Ikilinganishwa na bei zilizotangazwa tarehe 2 Machi 2022, bei ya rejareja ya mafuta yaliyopitia bandari ya Dar es Salaam imeongezeka kwa Sh 321 kwa lita moja ya petrol sawa na asilimia 12.65, dizeli Sh 289 sawa na asilimia 12.04 na mafuta ya taa Sh 473 sawa na asilimia 21.45.

Bei ya rejareja ya mafuta yaliyopitia bandari ya Tanga yameongeza kwa Sh 285 sawa na asilimia 11.12 kwa lita moja ya petroli na dizeli Sh 295 sawa na asilimia 11.90.

Bei ya rejareja ya mafuta yaliyopitia bandari ya Mtwara ambapo bandari hiyo imepokea mafuta ya dizeli pekee, imeongezeka kwa Sh 281 sawa na asilimia 11.12.

Mabadiliko ya bei hizo yamefanya bei za mafuta aina ya petrol kufikia Sh 2,861 kwa lita hadi Sh 3,105, dizeli Sh 2,692 kwa lita hadi Sh 2,936 na mafuta ya taa kufikia Sh 2,914 hadi Sh 2,925.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje, amesema mabadiliko ya bei hizo yamechangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta katika soko la dunia, gharama za usafirishaji na thamani ya Shilingi ikilinganishwa na Dola ya kimarekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!