Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaligomea kongamano la TCD
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yaligomea kongamano la TCD

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, kimesema hakitashiriki kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kikidai hakioni nia njema ya kukata kiu ya Watanzania kupata katiba mpya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Msimamo huo umetolewa leo Ijumaa, tarehe 18 Machi 2022, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati akitoa maazimio ya kikao cha Kamati Kuu ya Chadema, kilichofanyika hivi karibuni jijini humo.

Mkutano huo wa kitaifa wa haki, amani na maridhiano umepangwa kufanyika tarehe 30-31 Machi 2022 jijini Dodoma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

TCD ambayo kwa sasa inaongozwa na Mwenyekiti, Zitto Kabwe ni muunganiko wa vyama vitano vyenye wabunge bungeni na madiwani ambavyo, ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi, Chama Cha Wananchi (CUF) na Chadema.

Akizungumzia ushiriki wa Chadema kwenye kongamano hilo, Mbowe amesema hawatashiriki kwani wakati wa maandalizi na msingi wa maridhiano yanajengwa na kubainisha kasoro zinazowafanya kufanyiki kwa maridhiano tofauti nah apo hakutakuwa na tija.

“Kuhusu kongamano la TCD, tumeshauriana haya maridhiano yanayozungumzwa na TCD sisi hatujashirki kuandaa, viongozi walipitia taarifa kwanza na tukapitia yaliyopangwa. Tumeangalia vizuri tukasema hapana, hatushirki sababu hatuoni nia njema ya kutibu kiu ya Watanzania kuhusu katiba ,” amesema Mbowe.

Amesema “Chadema tumesema tutashiriki mazungumzo yote tunayoyaona yana nia njema kwa mtazamo wetu. Kwa mtazamo wetu kongamano linalopangwa Dodoma ajenda yake haizungumzii katiba mpya, inakwepa hoja ya katiba mpya.”

Katika hatua nyingine, Mbowe amesema Chadema hakitashiriki kongamano hilo, kwa kuwa baadhi ya wadau waliopangwa kutoa mada, walishiriki kuandaa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, akiwemo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa (NEC), Dk. Wilson Mahera ambaye atatoa mada.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)

“Miongoni mwa wawasilisha mada ni mtu anaitwa Mahera, mkurugenzi wa uchaguzi, huyo ndiyo akatuhubirie maridhiano? Tunapaswa kukaa kwanza na tuangalie tatizo liko wapi ndio twesonge mbele. Kwa hiyo sisi hatutakwenda,” amesema Mbowe

Mbowe amesema Chadema hakitaki katiba viraka bali kinahitaji katiba mpya itakayokata kiu ya Watanzania wote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!