CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakuna mtu anayeweza kuiendesha taasisi ya urais “kwa rimoti” na kwamba watu wanaofikiria hivyo “ni kuwa na mawazo finyu.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yameelezwa leo Ijumaa tarehe 18 Machi 2022 na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu fununu za wastaafu wa Urais kuwa nyuma ya yanayofanywa na Serikali.
Chongolo amesema urais si mtu bali ni taasisi na ndiyo yenye mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yanayofanyika nchini.
“Mtu ambaye anaweza kuonekana na upofu wa kiuongozi, ni yuke anayeweza kufikiria kwamba mamlaka ya urais yanaweza kuwa controlled (kuongozwa) kwa rimoti unakaa huku anasema kata kulia, kata kushoto. Urais ni taasisi ni ngumu sana taasisi ya urais kuongozwa kwa rimoti, mamlaka hayo ni ya Rais na si mtu mwingine yeyote, mimi Katibu Mkuu wa CCM lakini siwezi kuwa na hisia hata fikra kidogo kuwa naweza kuamulia mamlaka ya rais ya kufanya ninachotaka mimi,” amesema Chongolo.
https://www.youtube.com/watch?v=41yWIFhOQtc
“Sasa huyo ambaye anamadaraka makubwa kuliko sisi ambao ndio chama tawala nandio wenye kuongoza nchi yuko wapi, aje hapa atuambie yeye anatumia njia gani ya kushawishi maslahi yake kifanywe na mamlaka.
“Msione Rais halafu mkamwangalia hivi tu, mtu anayemwangalia rais kwa wasiwasi ana tatizo nab ado hajakomaa. Mtu yeyote anayejua Rais ni mkuu wa taasisi ya urais hawezi kuchezea taasisi na mamlaka yake. Yeye akinyanyua kalamu na kuishusha chini kuna watu hawalali kuhakikisha hayo mambo yanatokea,” amesema.
Grazie wasioelewa wamelewa