Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa kumwakilisha Rais Samia Qatar, Jordan
Habari za Siasa

Majaliwa kumwakilisha Rais Samia Qatar, Jordan

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameondoka nchini humo kwenda Qatar na Jordan kwa ziara ya kikazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akiwa huko, Majaliwa atamwakilisha Rais Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika vikao na viongozi wakuu wa nchi hizo.

Tanzania na Qatar zimepanga kuanzisha Tume ya Ushirikiano ya Pamoja ambayo itasimamia masuala mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo na usafiri wa anga.

Akiwa Jordan, waziri mkuu atashiriki mkutano wa kujadili usalama katika eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika hususan Msumbiji na maeneo jirani. Mkutano huo wa Aqaba Process on East Africa, utafanyika tarehe 24 Machi 2022 katika mji wa Aqaba, Jordan.

Mkutano huo ambao umeitishwa na Mfalme wa Jordan, Abdulla wa II ni wa tatu kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 na huwakutanisha viongozi wakuu wa nchi za ukanda wa Mashariki ya Afrika ili kujadili changamoto za ugaidi na namna ya kudhibiti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!