Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aibiwa pasipoti Ujerumani, amwomba nyingine Rais Samia
Habari za Siasa

Lissu aibiwa pasipoti Ujerumani, amwomba nyingine Rais Samia

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzania nchini Tanzania-Chadema, Tundu Lissu, amedai hati yake ya kusafiria (pasipoti), imeibiwa mwezi uliopita akiwa nchini Ujerumani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Lissu ametoa taarifa hiyo leo Alhamisi, tarehe 17 Februari 2022, akihojiwa kwa njia ya mtandao na Kituo cha Televisheni cha Azam, ambapo aliulizwa lini atarejea nchini Tanzania, akitokea uhamishoni Ubelgiji anakoishi.

Mwanasiasa huyo amesema jana Jumatano alipozungumza na Rais Samia Suluhu Hassan, jijini Brussels nchini Ubelgiji, alimueleza kwamba hana paspoti na kuwa anahitaji hati hiyo ya kusafiria.

“Sina hati ya kusafiria iliibiwa mwezi uliopita Ujerumani, nilimwabia sina pasipoti na nimefanya maombi nahitaji pasipoti. Kwa hiyo yakifanyika hayo nitakuwa njiani haraka sana, uhamishoni ni uhamisho tu,” amesema Lissu.

Lissu amesema, akipata paspoti pamoja na Rais Samia akitoa kauli ya kumtaka yeye na wenzake waishio uhamishoni warejee nyumbani akiwahakikishia usalama wao, atarejea haraka sana.

“Nimemwambia mheshimiwa Rais kwamba sisi tuliokimbia kwa sababu ya kuhofia maisha yetu na usalama wetu, tunahitaji assurance kwamba tukirudi nyumbani tutakuwa salama. Specifically nimemuomba Rais atukaribishe nyumbani,” amesema Lissu.

Makamu huyo Mwenyekiti wa Chadema Bara, amesema Rais Samia akitekeleza ombi lake hilo, hata dunia itaamini kwamba Serikali yake itahakikisha walioumizwa wakirejea Tanzania watakuwa salama.

“Atoe kauli yake kama Rais kwamba njooni nyumbani mtakuwa salama, hilo suala muhimu sana. Taifa likimsikia Rais amefanya hivyo na dunia ikisikia amesema hivyo, kutakuwa na imani,” amesema Lissu na kuongeza:

“Sio kwetu sisi na wale wanaoitakia mema nchi yetu watakuwa na imani kwamba sasa Serikali iko serious kuhakikisha watu wake walioumizwa vile wakirudi nyumbani watakuwa salama, likifanyika hilo mazingira ya safari yataanza mara moja,” amesema

Lissu yuko nchini Ubelgiji tangu Novemba 2020, aliporejea baada ya kumalizika kwa mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka huo, ambapo aligombea nafasi ya Urais, kupitia Chadema. Alirejea nchini humo alikokuwa akiishi tangu 2017, akidai amepata vitisho vya kiusalama.

Mwanasiasa huyo alikwenda Ubelgiji 2017, kupatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma.

Mbali na Lissu, mwanasiasa mwingine aliyekimbilia nje ya nchi akidai kuhofia usalama wa maisha yake ni Godbless Leman a Ezekiel Wenje wanayeishi uhamishoni nchini Canada, tangu 2020 baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo.

“Kama ilivyo kwangu, nimemweleza mheshimiwa Rais kwamba Godbless Leman a Wenje nao wako uhamishoni Canada, ni yeye sasa kutukaribisha na kutuhakikishia usalama wetu,” amesema

Katika taarifa iliyotolewa na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu jana Jumatano, alidai wawili hao walijadiliana masuala mbalimbali yenue maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1 Comment

  • I with due respct hope HE President Samia will accept that request and allow our patriots brothers to come back home and join forces to build our nation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!