Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari Mwanamke adaiwa kutolewa figo na mwajiri wake
HabariHabari Mchanganyiko

Mwanamke adaiwa kutolewa figo na mwajiri wake

Spread the love

 

MADAKTARI nchini Uganda wamethibitisha kuwa mwanamke aliyekuwa akifanya kazi za nyumbani nchini Saudi Arabia, aliondolewa figo yake ya kulia na sio ajali ya gari kama ilivyoarifiwa awali na mwajiri wake. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imethibitisha hilo baada ya kupewa ripoti ya uchunguzi kutoka Hospitali kuu ya taifa ya Mulago.

Kufuatia taarifa hiyo ya uchunguzi, familia ya mwanamke huyo imeiomba serikali kusimamia suala hilo hadi haki itakapopatikana.

Kwa mujibu wa BBC, Judith Nakintu mwenye umri wa miaka 38 ambaye pia ni mama wa watoto watano, alichukuliwa na kampuni ya Nile Treasure Gate mwaka 2019 kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za nyumbani huko Jeddah nchini Saudi Arabia.

Baada ya kufanya kazi karibu miezi miwili, mawasiliano yake na familia yake yalikatika, ndipo mama yake mzazi alipoanza kufuatilia karibu miezi mitatu ndipo akaambiwa mwanaye amepata ajali.

“Alitufahamisha kwa simu kwamba alipata ajali, nilikuwa nataka kufahamu familia yake, nikamuuuliza alipata ajali bila kampuni iliyompeleka kujua? Nikawapigia simu kampuni yake nikawaeleza, wakasema hawana habari wala taarifa,” alisema mama huyo.

Kampuni ya Nile Treasure Gate ilimpigia simu mama’ke Nakintu tarehe 30 Oktoba 2021 ambapo mwanaye alikuwa anatarajia kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebe siku hiyo.

Alielekea uwanja huo wa ndege kwa ajili ya kumpokea mwanae lakini alipowasili alimuona mwanae akiletwa kutoka kwenye ndege akiwa kwenye kiti cha wagonjwa cha magurudumu, hawezi kutembea na kuingizwa kwenye gari la wagonjwa hadi Hospitali kuu ya Mulago.

Kesho yake wakaruhusiwa kwenda nyumbani, lakini yeye hakuamini ripoti aliyopewa.

“Tulipolala hospitali maafisa wa kampuni waliyomchukua wakamleta daktari kufanya uchunguzi wa kitabibu wakasema yupo sawa hana tatizo, mimi sikuridhishwa, siku ya Jumatatu nikarudi Mulago wakamfanyia uchunguzi upya nikaambiwa figo moja imetolewa,” alisema mama huyo.

Afisa mratibu wa kuzuia ulanguzi wa binadamu kutoka Idara ya Uhamiaji Uganda, Agness Igoye, amewaeleza waandishi wa habari kwamba, Hospitali kuu ya Mulago imethibitisha kwamba alitolewa figo moja.

Uchunguzi wa madaktari nchini Uganda umethibitisha figo yake ya kulia ilitolewa, uchunguzi wa awali wa Polisi umetambua muajiri wake wa nchini Saudi Arabia kwa jina la Sadaffa Muhamed, alitoa ripoti bandia za kitabibu kuwadanganya wanafamilia ya muathiriwa.

Zilionyesha sehemu zake zote za viungo zipo sawa wakati sio kweli.

Ripoti ya awali kutoka Polisi wa Saudi Arabia zilionyesha Nakintu ambaye amepooza, alipata ajali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na mtandao wa Indepent nchini Uganda, Kampuni ya Nile Treasurer, siku chache baadaye ilipokea taarifa kuwa watoto wawili wa waajiri hao wamefariki dunia kutokana na ajali hiyo, bahati nzuri Nakintu alinusurika ingawa ameumia sana na kusababisha damu yake kuganda.

Kwa upande wake, Rais wa Migrant Workers Voice, inayoshughulikia masuala ya wafanyakazi wahamiaji, Abdallah Kayonde, amesema ameiandikia Kampuni hiyo kulipa fidia ya shilingi milioni 600 za Uganda kwa kitendo cha kutolewa figo ya muathirika huyo kinyume cha sheria na kuuzwa.

Hata hivyo, Kampuni hiyo imenukuliwa ikipinga kuhusika na kutolewa kwa figo ya mwanamke huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!