Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba, ASEC kuchimbika kombe la Shirikisho
Michezo

Simba, ASEC kuchimbika kombe la Shirikisho

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba itashuka dimbani Jumapili tarehe 13, dhidi ya ASEC Mimosas, kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika huku kila timu ikiwa kwenye kiwango bora kwa sasa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kundi D, utapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, majira ya saa 11 jioni, huku mashabiki 35,000 wakitarajiwa kuwa sehemu ya mchezo huo mara baada ya kupata ruhusu kutoka ndani ya Shirikisho la Mpira Barani Afrika (CAF)

Timu hizo zote mbili zitashuka dimbani, kwenye mchezo ambao utakuwa na mvutano mkubwa kutokana na ubora wa wachezaji kwa pande zote mbili na kufanya vizuri kwenye Ligi za nchini mwao.

ASEC ambao wanashiriki Ligi Kuu nchini Ivory Coast, wanakuja kucheza na Simba kwenye mchezo huo, huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi ya nchini kwao.

Katika msimamo wa Ligi hiyo ASEC wanashikilia nafasi ya kwanza, wakiwa na pointi 21, mara baada ya kucheza michezo saba huku wakiwa hawajapoteza mechi yoyoye.

Aidha katika michezo hiyo, timu hiyo imepachika jumla ya mabao 23, huku ikiruhusu nyavu zao kutikiswa mara tatu na kufanya utofauti wa mabao kuwa 10.

Kwa upande wa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mpaka sasa wao wamecheza jumla ya michezo 15 wakiwa kwenye nafasi ya pili na jumla ya pointi 31.

Katika michezo hiyo Simba mpaka sasa wamepachika jumla ya mabao 16, huku wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara sita kwenye michezo yote waliocheza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

error: Content is protected !!