Spread the love

 

KLABU ya soka ya Yanga imeibuka na kulalamikia mwenendo wa waamuzi kwa baadhi ya michezo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na kutaka mamlaka ya soka nchini kuliangalia jambo hilo kwa ukaribu ili kupata bingwa atakayepatikana kwa haki. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Yanga wameibuka ikiwa ni siku chache toka kulaumiwa kwa refa aliyecheza mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba dhidi ya Mbeya Kwanza kwa kukubali bao lililoonekana kuwa ni la kuotea.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo tarehe 8 Februari 2022 kwenye makao makuu ya klabu hiyo, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema kuwa kuna baadhi ya maamuzi ambayo yanaonekana kunufaisha baadhi ya timu na kuumiza timu nyingine.

“Kumekuwa na mlolongo wa matukio ya maamuzi yenye utata ambayo kwa namna moja au nyingine yananyima haki ya timu zingine na yanatoa manufaa kwa timu zingine,”Alisema Bumbuli.

Bumbuli aliendelea kwa kuzitaka mamlaka zinazosimamia soka nchini ambazo ni Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) na bodi ya Ligi kuhakikisha wanachukua hatua kwa wjuu ya matukio hayo.

“Tunataka Waamuzi wetu waanze kujitafakari juu ya haya ambayo yamekuwa yakiendelea na yamekuwa mjadala mkubwa sana kwenye Taifa letu, Lakini pia tunataja mamlaka zinazosimamia mpira zichukue hatua juu ya jambo hili ambalo watu wamewekeza pesa zao”Alisiitiza Bumbuli

Kwa upande wa msemaji wa klabu hiyo ambaop ni vinara wa Ligi Kuu mpaka sasa, Haji Manara kwa upande wake alitaka haki itendeke kwa kila upande, licha ya kuona kwa upande wao wanaadhibiwa kila wakifanya makosa lakini ni tofauti inavyokuwa kwa upande wa Simba.

“Tunataka kuwa waamuzi kuwa na haki kwanini Yanga ikifanya makosa iadhibiwe lakini wenzetu pia Simba wakifanya makosa basi haki itendeke kwanini wao wakifanya makosa haki haitendeki.” Alisema msemaji huyo

Aidha aliendelea kwa kusema kuwa, katika mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza, wapinzani wa karibu kwenye msimamo huo ambao ni Simba walionekana kama wamepewa bao la upendelea kufuatia mchezaji wao kuonekana ameotea.

“Mechi na Mbeya kwanza wenzetu wamepewa Goli la wazi kabisa na mchezaji alikuwa amezidi lakini Mwamuzi akaruhusu goli sasa haki iko wapi.” Alisema Haji.

Yanga ambao wanatarajia kushuka tena dimbani kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, tarehe 22 Februari kuwakabili Mtibwa Sugar, mchezo utakaopigwa majira ya saa 10 kamili kwenye dimba la Manungo, Turiani mkoani Morogoro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *