Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kina Mbowe wahoji jalada kufunguliwa bila maelezo
Habari za SiasaTangulizi

Kina Mbowe wahoji jalada kufunguliwa bila maelezo

Spread the love

 

TUMAIN Swila, Shahidi wa 13 wa Jamhuri katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu amedai wakati anafungua jalada la kesi hiyo, hakuchukua maelezo ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Boaz, kwa kuwa sio lazima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Swila ambaye ni inspekta wa Polisi, ametoa madai hayo leo Jumanne, tarehe 7 Februari 2022, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumi Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga, akiulizwa maswali ya dodoso na Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi, Peter Kibatala.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni waliokuwa makomando wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Kibatala alimhoji Inspekta Swila kwa nini alifungua jalada la kesi hiyo bila ya maelezo ya DCI mstaafu Boaz, aliyekuwa mlalamikaji katika taarifa hiyo, ambapo alijibu akidai haikuwa na ulazima.

Mahojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo;

Kibatala: Unasema ulifungua IR/CD/ 2097/ 2020, tarehe 18 Julai 2020?

Shahidi: Ndiyo.

Kibatala: Ulikuwa hukuchukua maelezo ya malalamikaji Robert Boaz?

Shahidi: Sio lazima.

Kibatala: Ni kweli ulifungua jalada bila ya kuwa na maelezo ya mlalamikaji?

Shahidi: Nimejibu hilo swali, kwamba ni kweli lakini haina ulazima.

Kibatala: Unafahamu maelezo ya Boaz yaliandikwa chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai?

Shahidi: Labda nirejee.

Kibatala: Tarehe 13 Oktoba 2020, maelezo ya Boaz yaliandikwa, unafahamu Boaz yaliandika chini ya kifungu cha 10 (3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai?

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Kwa mujibu wa sheria, afisa anayepokea taarifa za uhalifu inatakiwa mapema iwezekanavyo a-reduce hiyo taarifa kwa maandishi, unafahamu?

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Ulivyosema sio lazima uwe unafungua faili bila maelezo ya mlalamikaji au mtoa taarifa ulikuwa una maanisha nini?

Shahidi: Ile taarifa unaifungua kwenye kitabu iwe RB ndiyo umeshaandika maelezo pale.

Kibatala: Unachotaka kutuambia unaweza kuandika taarifa ya kujwruhi bila maelezo ya yule aliyejeruhiwa?

Shahidi: Kuna mazingira inawezekana.

Wakati huo huo, Inspekta Swila amedai kesi hiyo sio ya kutungwa, baada ya Wakili Kibatala kuhoji kwa nini watu wasione kesi hiyo ni ya kutungwa, akidai maelezo ya mlalamikaji yameandikwa baada ya jalada hilo kufunguliwa.

Kibatala: Tumekubaliana umefungua faili huna maelezo ya mlalamikaji, tueleze maelezo ya DCI yaliandikwa tarehe gani?

Shahidi: Sikumbuki.

Kibatala: Nakuonesha kama ni kweli haya maelezo yalindikwa tarehe 13 Oktoba 2020?

Shahidi: Yameandikwa tarehe 13 Oktoba.

Kibatala: Ambayo ni miezi mingapi tangu wewe kufungua jalada bila maelezo ya mlalamikaji?

Shahidi: Karibia miezi mitatu.

Kibatala: Maelezo ya mlalamikaji anatoa amri huku na huku yamendikwa miezi mitatu toka faili lifunguliwe, mnataka tuone kesi hi sio ya kutungwa shahidi?

Shahidi: Sio ya kutungwa.

Kibatala: Maelezo ya mtoa taarifa aliyemwambia DCI kuwa Mbowe kamwambia yeye, halafu yeye kamwambia DCI, umeanidika tarehe ngapi?

Shahidi: 11 Agosti 2020

Kibatala: Ambayo ilikuwa muda gani tangu umefungua faili tarehe 18 Julai 2020?

Shahidi: Wiki tatu.

Kibatala: Kwa fact hizi kwa nini tusiamini njama washtakiwa wanasema Urio alikamatwa, alikamatwa baada ya kutajwa na Adam na Ling’wenya kwamba wao ndiyo waliwapeleka kwa Mbowe, akapigwa mkapa dili la kuwa shahidi?

Shahidi: Sio kweli, kuchelewa kuandikwa kwake maelezo kama shahidi haimaanishi kesi sio ya kweli.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita ya ugaidi, ikiwemo kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi, kudhuru viongozi wa Serikali, kulipua vituo vya mafuta na maeneo yenye mikusanyiko ya watu, kupanga maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai na Agosti 2020, kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Kilimanjaro.

Inspekta Swila anendelea kutoa ushahidi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!