Tuesday , 30 April 2024
Home Kitengo Michezo Mastaa Kylie, Travis Scott wapata mtoto wa pili
Michezo

Mastaa Kylie, Travis Scott wapata mtoto wa pili

Spread the love

Mwanamitindo na mfanyabiashara kutoka Marekani, Kylie Jenner (24) pamoja na mpenzi wake ambaye ni Msanii wa rap, Jacques Bermon Webster maarufu kama Travis Scott (30) wametangaza rasmi ujio wa mtoto wao wa pili. Anaripoti Glory Massamu (endelea).

Hayo yamejiri leo tarehe 7 Februari, 2022, huko Marekani baada ya mwanamitindo huyo kuweka picha katika mtandao wake wa Instagram zinazomuonesha mtoto wake Stormi anayeonekana akiwa ameshika mkono wa mtoto mchanga.

Hata hivyo, mtoto huyo anakuwa ni wa pili kwa wapenzi hao ambao ni maarufu duniani baada ya Stormi Webster (4) aliyezaliwa Februari, 2018.

Mwanamitindo huyo ni moja kati ya wanawake maarufu na wenye mafanikio makubwa duniani huku akiwa na umri mdogo, kwani Jenner aliwekwa kwenye orodha ya jarida la Forbes na kumfanya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuangaziwa kwenye orodha hiyo.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes 2019, utajiri wa Jenner ulikadiriwa kuwa dola za Marekani bilioni moja, ingawa suala hilo lilileta utata baadaye na kuhisiwa kwamba ni upendeleo ulifanyika.

Mei mwaka 2020 Forbes ilitoa taarifa zikimtuhumu Jenner kwa kughushi hati za ushuru ili aonekane kama bilionea pia lilimshtaki kwa kutengeneza takwimu hizo.

Hata hivyo, Kylie Jenner bado anaonekana ni mwanamke mwenye mafanikio hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa anaoufanya kwenye biashara yake ya vipodozi ya (Kylie Cosmetics).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!