Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Senegal yatangaza mapumziko baada ya kushinda Afcon
KimataifaMichezo

Senegal yatangaza mapumziko baada ya kushinda Afcon

Spread the love

 

RAIS wa Senegal, Macky Sall ametangaza leo Jumatatu tarehe 7 Februari, 2022 kuwa siku ya mapumziko kusherehekea ushindi wa timu ya taifa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Sall ambaye alikuwa nje ya nchi amefutilia mbali awamu ya mwisho ya safari yake katika Visiwa vya Comoro na kurejea nchini mwake kuwapokea nyota hao wa soka kurejea nchini leo.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Taifa – RTS, Rais Sall pia kesho Jumanne ataiandalia dhifa maalumu Ikulu.

Senegal imeshinda fainali ya kwanza ya Afcon baada ya kushindwa mara mbili katika fainali za mwaka 2002 na 2019.

Waliishinda Misri 4-2 kwa mikwaju ya penalti na kupata ushindi wao baada ya fainali kumalizika bila bao kufuatia muda wa nyongeza.

Wakati huo huo, raia wameendelea kusherehekea usiku kucha kuamkia leo Jumatatu katika miji mbalimbali nchini Senegal kufuatia ushindia wa Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kocha wa Senegal Aliou Cissé kipindi akiwa mchezaji alikosa penalti muhimu fainali za mwaka 2002 na kushindwa kubeba kombe hilo la Afcon.

Akiwa kama kocha, timu hiyo ilishindwa katika fainali ya mwaka 2019.

Senegal na Misri zitakutana tena katika mechi nyingine mwezi ujao kwenye mchujo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!