Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Mwigulu aja na wazo la VAR 
Michezo

Mwigulu aja na wazo la VAR 

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amefunguka kuwa katika bajeti  ijayo ya Serikali atashauliana na Waziri mwenye dhamana ya michezo Mohammed Mchengelwa, kuhakikisha waanaweka teknolojia ya kufanya maamuzi kwa njia ya video “VAR’ kwa viwanja 10. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mwigulu amenena hayo kufuatia baadhi ya waamuzi wanaochezesha michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kushindwa kufanya maamuzi sahihi kwenye baadhi ya michezo na kuumiza baadhi ya timu.

Waziri huyo ameyanena hayo kupitia andiko lake kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, huku akiwa ameambatanisha na kipande cha video ambacho mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Mbeya City alitafsiri kuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga Fiston Mayele kuwa alikuwa kwenye eneo la kuotea.

Katika andiko hilo Waziri huyo aliandika kuwa, katika bajeti ijayo ya serikali atashauliana na waziri wa michezo kuweka teknolojia hiyo ya VAR, sambamba na kuweka nyasi bandia kwenye baadhi ya viwanja ambavyo vinaonekana havipo kwenye hali nzuri.

Nitashauriana na Waziri mwenzangu anayesimamia Michezo, bajeti ijayo tumtafutie Fedha, Tuweke VAR viwanja hata 10, tuweke nyasi bandia kuondoa utaratibu wa kucheza football shambani. Haya ndio maeneo yanayolalamikiwa.” Aliandika Mwigulu

Hivi karibuni baadhi ya waamuzi wamefungiwa na kamati ya uwendeshaji na usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) kufuatia kushindwa kutafsili vizuri sharia 17 za mchezo wa mpira wa miguu na baadhi ya waamuzi wameonekana kupitwa na matukio mengi kiasi cha kuumiza baadhi ya timu.

Teknolojia hiyo ya VAR kwa mara ya kwanza ilianza kutumika kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2018, nchini Ufaransa na sasa inatumika katika Ligi Kubwa tano duniani.

Kwa habari zaidi, soma gazeti la Raia Mwema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!