Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia azuru kaburi Mwalimu Nyerere
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia azuru kaburi Mwalimu Nyerere

Rais Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Julias Nyerere
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan leo tarehe 7 Februari 2022 amezuru kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere nyumbani kwake Butiama mkoani Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Rais Samia ambaye ameongozana na mawaziri, manaibu mawaziri, wabunge na viongozi wengine wa CCM, amepokewa na mtoto wa Mwalimu Nyerere, Makongoro Nyerere kisha kuelekea katika chumba maalumu kulipohifadhiwa mwili huo na kumuombea dua.

Mbali na kusaini kitabu cha wageni, pia alipita katika makumbusho ya Mwalimu Nyerere ambako mtoto mwingine wa Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere alimpokea akiwa ameambatana na aliyekuwa Katibu wa Nyerere, Joseph Butiku.

Akizungumza ndani ya makumbusho hayo, Rais Samia amesema mbali na kwenda kuisalimia familia hiyo ya Mwalimu Nyerere pia amewashukuru wananchi wa mkoa wa Mara kwa kufanikisha maadhimisho ya miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Mungu alitushushia mja ambaye alimpa maono ya kuunda Taifa hili na kutuwekea misingi ambayo tunaitumia hadi leo katika kuendesha Taifa letu. Sisi kwetu ni kumshukuru Mungu na neema zake kwa kutushushia mja huyu na tukija duniani.

“Tunamshukuru Baba wa Taifa kwa kazi kubwa aliyoifanya kiasi ambacho miaka mingi baadaye sisi tumeingia lakini tunatumia misingi ileile kuendesha nchi yetu na nchi inakwenda vizuri.

Tunashukuru wana-Butiama wote kwa mchango wetu katika Taifa hili,” amesema Rais Samia.

Awali akizungumza na wananchi wa Butiama mkoani humo, ametaja sababu za maadhimisho hayo ya miaka 45 ya CCM kufanyika mkoani Mara.

“Tumemaliza sherehe za miaka 45 ya CCM ambacho ni chama kilichoasisiwa na Baba wetu wa Taifa – Mwalimu Nyerere ambaye ni zao la Butiama. Angekuwepo tungeadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwake.

“Lakini kwa sababu hayupo tukasema tuadhimishe na tutoe heshima ya miaka 45 ya CCM maadhimisho yafanyike huku Mara na tufike huku Butiama kuja kusalimia na hilo ndilo tulilolifanya. Nawashukuru sana kwa mkutano huu,” amesema Rais Samia.

Aidha, amesema maendeleo yaliyoletwa Serikali chini ya CCM, yameanzia awamu ya Baba ya Taifa.

Ameahidi wananchi kwamba Serikali itaendelea kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

“Ili tuwe na fedha nyingi za maendeleo, inabidi kufanya kazi kwa bidii tupate fedha na maendeleo yaende kwa wananchi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!