MARA baada ya Timu ya Taifa ya Senegal kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la Mataifa Afrika (AFCON), Rais wa nchi hiyo Macky Sall ametangaza kuwa siku ya leo ya Jumatatu ya tarehe 7 Februari kuwa ni mapumziko nchi nzima. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Senegal wametwaa ubingwa huo, mara baada ya kuifunga tmu ya Taifa ya Misri, kwa mikwaju ya penati 4-2, kufuatoia kutoshana nguvu kwenye dakika 120 za mchezo.
Rais Sall ametangaza siku hii kuwa ya mapumziko ili kusherehekea ushindi huo, mara baada ya kucheza fainali tatu za michuano hiyo na kutoka kapa.
Kikosi hiko cha Senegal kinatarajia kurejea leo nchini mwao wakitokea Cameroon walipokuwa wakishiriki michuano hiyo.
Licha ya kutwaa taji hilo, Senegal wamefanikiwa kutoa kipa bora wa michuano hiyo ambae ni Édouard Mendy, mchezaji bora wa fainali hizo ambaye tuzo hiyo imekwenda kwa Sadio Mane na pia kocha mkuu wa kikosi hiko Aliou Cisse ametwaa tuzo ya kocha bora wa michuano hiyo.
Leave a comment