Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa KUELEKEA AFCON: Cheki mchezaji alivyoagwa na mkewe kwa mabusu ‘mubashara’
KimataifaMichezo

KUELEKEA AFCON: Cheki mchezaji alivyoagwa na mkewe kwa mabusu ‘mubashara’

Spread the love

 

Musah Noah Kamara, mchezaji kandanda wa Sierra Leone, ameagwa kwa mapenzi na bashasha la kipekee kutoka kwa mkewe wakati akijiandaa kuelekea katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2021 yanayotarajiwa kufanyika huko nchini Cameroon. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mshambuliaji huyo hatari maarufu Musa Tombo, akipigwa mabusu miguuni na mkewe, ikiwa ni baraka za kipekee na kumuaga mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa maarufu kama ‘Bo Rangers’.

Kitendo hicho cha mkewe huyo anayefahamika kwa jina la Hawa Kamara (miaka 21) kimevunja rekodi mitandao huku wachangaji wengi wakisema ni ishara bora ya unyenyekevu na upendo aliyoionesha Hawa kwa mumewe huyo.

Musa Tombo ni miongoni mwa wachezaji 28 watakaoiwakilisha Sierra Leone nchi ambayo imerejea katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kusota kwa miaka 26.

Mashindano hayo yanayoshirikisha mataifa 24 yamepangwa kufanyika kati ya Januari 9 hadi Februari 5 nchini Cameroon.

Michezo hiyo itachezwa katika miji mitano ambayo ni Yaounde (uwanja wa Olembe na Stade Ahmadu Ahidjo); Douala (uwanja wa Japoma); Garoua (uwanja wa Roumde Adjia); Bafoussam (uwanja wa Kouekong) na Limbe (uwanja wa Limbe).

Sierra Leone ipo Kundi E na itacheza dhidi ya Algeria, Ivory Coast na Equatorial Guniea.

Karata yake ya kwanza itarushwa Jumanne tarehe 11 Januri, Jumapili tarehe 16 Januari na Alhamisi tarehe 20 Januari. Michuano hiyo itakamilika Jumapili, tarehe 6 Februari mwaka huu.

ALIIKACHA SWEDEN KISA BARIDI

Licha ya kwamba wachezaji wengi wa Kiafrika ndoto zao ni kucheza soka la kulipwa Barani Ulaya, kwake Tombo hilo halikuwa kipuambele kwani aliikacha klabu moja huko Sweden sababu ya baridi kali.

Mwaka 2018 mchezaji huyo aliyekuwa akisakata kandanda katika klabu ya AIK Freetong iliyokuwa ikishiriki ligi kuu nchini Sierra Leone, aliibuka kinara wa mabao pamoja na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa.

Mafanikio hayo yalimwezesha kusajiliwa katika klabu ya Trelleborgs FF ya nchini Sweden kwa mkataba mnono wa miaka mitatu na nusu lakini cha ajabu mwaka 2019 alivunja mkataba huo na kurejea nyumbani Sierra Leone sababu hali ya hewa kuwa ya baridi kali.

Mwaka huo huo 2019 – 2020 alijiunga na Klabu ya Hadiya Hossana ya nchini Ethiopia na mwaka 2020 hadi sas anakipiga katika klabu ya nyumbani ya East End Lions.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

error: Content is protected !!