November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mapenzi yashinda! Mwimba injili amuoa mpenziwe ‘bibi kizee’

Spread the love

 

WAHENGA husema kipendacho roho hula nyama mbichi na miaka si chochote wala lolote mbele ya mapenzi, miaka ni namba tu.

Hilo limejitokeza kwa Msanii wa muziki wa nyimbo za injili nchini Kenya, Peter Omwaka maarufu kama Guardian Angel na mpenzi wake Esther Musila ambaye mapema wiki hii wamefunga ndoa rasmi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wawili hao walifanya harusi ya faragha iliyohudhuriwa na wanafamilia na marafiki wachache tarehe 4 mwezi Januari, 2022

Guardian Angel mwenye umri wa miaka 31 na Musila (miaka 51) waliibua gumzo nchini humo baada ya uhusiano wao kuwa wa wazi huku wengi wakiukosoa kwa sababu ya utofauti wa ukati ya wawili hao.

Hata hivyo, baada ya kufunga ndoa hiyo, walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kufahamisha walimwengu kuhusu hatua hiyo muhimu ambayo wameipiga.

“Na katika siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwangu, Mungu alinitendea tena. Bw na Bi Omwaka… mke wangu @esther.musila” Guardian Angel aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Bi Musila alisherehekea hatua waliyopiga na mpenzi wake huku akimtaja mwanamuziki huyo kama mtu maalum na rafiki wake wa dhati.

Kwenye chapisho lake Instagram, Malkia huyo mwenye umri wa miaka 51 alikiri kamwe maishani hakuwahi kufikiria kwamba angepakutana na mpenzi kama Guardian Angel.

“Kupata mtu maalum kama wewe kati ya watu wote ulimwenguni ni jambo ambalo sikuwahi kufikiria. Acha tufanye maisha haya pamoja. Bw na Bi Omwaka” Esther aliandika.

Wanandoa hao wawili wamekuwa katika mahusiano kwa kipindi cha takriban miaka miwili na wamekuwa wakijivunia maamuzi waliyofanya ya kuwa pamoja licha ya ukosoaji mkubwa ambao wamekabiliana nao kufuatia pengo kubwa kati ya umri wao.

Esther ana watoto wawili wakubwa kutoka kwa ndoa yake ya awali. Aliyekuwa mume wake na ambaye ni baba ya watoto wake watatu aliaga dunia takriban miaka mitano iliyopita.

Wanawame mwanamama huyo, Gilda Naibei Musila na Glen Musila walisema walimpokea Guardian Angel vizuri alipojiunga na familia yao.

Wawili hao walisema waliridhishwa na namna msanii huyo alijiunga na familia yao huku wakieleza kwamba hakujitambulisha kama baba wa kambo ila kama rafiki.

“Yeye ni kama mshauri. Yeye ni rafiki. Hatuwezi sema yeye ni kama baba, anajaribu kuwa baba. Sababu moja tulielewana vizuri na yeye ni kwa sababu hakuja na fujo akisema eti atakuwa baba yetu wa kambo na kuharibu kila kitu. Alikuja kama rafiki na kusema tunaweza kuzungumza naye kuhusu kitu chochote” alisema Gilda.

error: Content is protected !!