Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Baba mbaroni kwa kujaribu kumuuza mwanawe
Kimataifa

Baba mbaroni kwa kujaribu kumuuza mwanawe

Spread the love

 

POLISI nchini Liberia wamemkamata na kumfungulia mashtaka mwanamume mmoja raia wa Sierra Leone mwenye umri wa miaka 29 kwa madai ya kujaribu kumuuza mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 10. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Inaonekana ilikuwa ni jitihada ya kutafuta pesa za kununua pikipiki mpya baada ya aliyokuwa nayo kuibwa.

Baada ya kukamatwa, mwanaume huyo aliwaambia maofisa wa uchunguzi katika mji mkuu, Monrovia, kwamba alihitaji karibu $1,000 (Sh milioni 2.3) kwani pikipiki hiyo, ambayo ilikuwa ya rafiki yake, ilikuwa imeibiwa nyumbani kwake.

Aliambiwa njia pekee ya kupata pesa nyingi hivi haraka ni kwenda nchi jirani ya Liberia kujaribu kutafuta mnunuzi wa mtoto wake.

Nyumbani kwao watu walikuwa wamemwambia itakuwa rahisi kufanya mauzo ya aina hiyo katika eneo la mpakani.

Ilipangwa kupitia mtu wa kati mnamo Desemba. Wakati wa mazungumzo mvulana huyo alijulikana kama kuku na sio binadamu ili kuepusha kugunduliwa.

Hata hivyo, polisi walipokea taarifa na babake akakamatwa kwani mnunuzi aliripotiwa kuwa njiani kumchukua mvulana huyo kutoka mji nje ya Monrovia.

Kulingana na chapisho la mtandaoni la Liberia Global News Network, mtoto huyo kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa wizara ya jinsia.

Ulanguzi wa binadamu ni suala kubwa katika Afrika Magharibi.

Watoto wanaouzwa katika utumwa wa kisasa hawaruhusiwi kuwasiliana na familia zao na mara nyingi wanalazimishwa kufanya kazi kama watumishi wa nyumbani au vibaru

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!