Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TCRA yaishushia rungu Wasafi TV
Habari Mchanganyiko

TCRA yaishushia rungu Wasafi TV

Spread the love

 

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeipa adhabu Kampuni ya Wasafi Televisheni Limited (Wasafi TV) ya kuomba radhi mara tatu kwa siku na kulipa faini ya Sh.2 milioni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya kukutwa na hatia katika kosa la kukiuka Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni 2020, kwa kurusha maudhui yenye kukashifu na kupotosha dini ya Kikristo.

Uamuzi wa kamati hiyo umesomwa leo Jumatano, tarehe 22 Desemba 2021 na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TCRA, Hans Gunze, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Gunze amesema, kamati hiyo imeipa onyo Kampuni ya Wasafi TV, pamoja na kuitaka iombe radhi mara tatu kwa siku, kuanzia kesho Alhamisi hadi Jumamosi ya tarehe 25 Desemba 2021, huku ikiiamuru ilipe faini ya Sh. 2 Milioni, ndani ya siku 21 tangu siku ya kutolewa adhabu hiyo.

“Baada ya kutafakari kwa kina maelezo yaliyowasilishwa na Wasafi TV, kamati ya maudhui imeridhika pasipokuwa na shaka kuwa, Wasafi TV kupitia kipindi chake tajwa cha ‘Hata Yesu alifuata wenye pesa, msituite matapeli’ zimekiuka Kanuni za Mawaisliano yaKielektroniki na Posta na Maudhui ya Mtandaoni ya 2020,” amesema Gunze.

Gunze amesema ‘kwa mujibu w a kanuni ya 21 (3 A, B, D) ya kanuni tajwa, kamati inatoa adhabu zifuatazo, wanapewa onyo kali.”

“Pili, imeamriwa waombe radhi watazamaji wake na umma kwa ujumla, kupitia kituo chake cha Wasafi TV na chaneli za mtandoani, ambazo zilitumika kurusha maudhui hayo na ifanywe hivyo mara tatu, kila siku na kila baada ya saa nne kwa saa za mchana,” amesema

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Maadili ya TCRA, amesema kampuni hiyo imeadhibiwa baada ya kukutwa na hatia katika kosa hilo, kufuatia mgeni wake, Nabii Daniel Shillah, kudai ‘Yesu ni tapeli wa kwanza duniani’.

Aidha, Gunze amesema, kampuni hiyo ina nafasi ya kukata rufaa katika Baraza la Ushindani (FCT), ndani ya siku 21 kuanzia leo.

Gunze amesema, kosa hilo lilitendeka tarehe 1 Novemba 2021, kupitia mahojiano ya mtangazaji wake, Jordan Mwasha na Nabii Shillah, ambapo inadaiwa mtangazaji huyo aliendelea kumhoji nabii huyo, licha ya kutoa kauli zenye ukakasi.

“Nabii Shillah aliongea maudhui yenye lugha ya upotoshaji, isiyo na staha, yenye kukashifu imani ya kikristo.”

“Kiuhalisia kimerushwa pasio kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya uandishi na utangazaji wa habari. Mtangazaji aliendelea kumhoji hata pale alipotamka maneno yenye ukakasi, kufuru, kashfa na yenye kuidhalilisha dini,” amesema Gunze na kuongeza:

“Kwa kusema kuwa Yesu ndiyo tapeli wa kwanza duniani, ambaye alifanya wizi wa wazi kwa kumtumia mwanafunzi wake kuiba punda katika Mji wa Yerusalemu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!