Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Balozi Kiondo atajwa sakata la ununuzi wa meli
Habari za SiasaTangulizi

Balozi Kiondo atajwa sakata la ununuzi wa meli

Balozi Kiondo akiagana na Rais Recep Tayyip Erdoǧan, baada ya kufanya mazungumzo kuhusu mahusiano ya Tanzania na Uturuki
Spread the love

 

SAKATA la zabuni za ujenzi wa meli mpya tano, iliyotolewa na Serikali ya Tanzania kwa kampuni mbili kutoka nchini Uturuki, limeanza kuchukua sura mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje, ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki na wizara ya ujenzi na uchukuzi, zinamtaja aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini humo, Profesa Elizabeth Kiondo, kwamba ndiye aliyepewa kazi ya kufanya uhakiki wa kampuni zilizoomba zabuni.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Shirika la Taifa la Meli (MSCL), liliwasilisha maombi rasmi kwa wizara ya mambo ya nje, kuomba kusaidia kupatikana kwa taarifa juu ya uwezo, hadhi na sifa za makampuni mawili yaliyoshinda zabuni, kupitia ubalozi wake nchini Uturuki.

Kampuni ambazo zimeshinda zabuni na ambazo kampuni ya meli ilitaka zifanyiwe uchunguzi, ni M/S Yutek Gemi Insa.Ltd (Mbia Mkuu) na JV Arti Muhendisk Insaat Taahhut Gemi Sanayi-ve Ticaret LTD STI.

Kwa taarifa kamili, soma gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Jumatano – Mhariri.

1 Comment

  • Duh!
    Je, ni kweli waafrika tunahongeka kirahisi?
    Mwalimu Nyerere aliyah kuonya kwamba, “wapo watu, wanadiriki kutaka kuwauza mama zao.”
    Hii inatufundisha kuwa wengi wetu bado tuna upeo mfupi wa akili. Upeo mfupi, unatufanya tufikirie ngazi ya ubinafsi na umimi. Hiyo ikitimizwa, tunaishia kwenye familia…basi.
    Hatujali chochote zaidi ya hapo…huu ni upeo mfupi unaotufanya tuhongeke kirahisi na kuacha utaifa.
    Tuanze kuwaondoa viongozi wenye kashfa za aina hii. Kwani walipaswa kuifanya kazi yao kwa weledi na uadilifu. Sasa huyu ni msomi na profesa lakini ana upeo mfupi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!