Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Tangulizi ACT-Wazalendo: Tunasubiri mjadala tume huru ya uchaguzi
Tangulizi

ACT-Wazalendo: Tunasubiri mjadala tume huru ya uchaguzi

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akizungumza na wanachana wa chama hicho katika jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma.
Spread the love

 

CHAMA cha siasa cha upinzani nchini Tanzania cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema, wanasubiri mjadala wa kitaifa kuhusu aina ya Tume Huru ya Uchaguzi “tunayoihitaji.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma … (endelea).

Hayo yamesemwa jana Jumanne, tarehe 21 Desemba 2021 na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, alipokuwa akizungumza na viongozi wa chama hicho Jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma.

Ni katika mwendelezo wa ziara yake mikoa ya Ruvuma, Selous, Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga yenye lengo la ujenzi wa chama, kuhamasisha na kufanya harambee ya michango ya wanachama ya kugharamia Mkutano Mkuu wa Chama wa tarehe 29 Januari 2022.

Pia, kufafanua mageuzi ya uendeshaji Chama kisayansi yanayotarajiwa kuzinduliwa kwenye Mkutano Mkuu huo.

Ado alisema, ofisi yake imeiagiza ofisi ya mwanasheria mkuu wa chama hicho kuanza mchakato wa kukusanya maoni ya wanachama kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi inayotakiwa na ACT Wazalendo.

“Kwenye kikao cha wadau wa siasa juu ya hali ya demokrasia nchini kilichofanyika Dodoma, suala la Tume Huru ya Uchaguzi liliafikiwa na pande zote.”

“Kwetu sisi ACT Wazalendo, hatua inayofuata ni mjadala wa kitaifa kuhusu aina ya Tume Huru tunayoihitaji” alisema Ado

Katibu mkuu huyo alisema, vikao vya ACT Wazalendo (Kamati Kuu ya Juni na Halmashauri Kuu ya Oktoba 2021) vimeagiza chama kulipa kipaumbele suala la Tume Huru ya Uchaguzi.

Ado alisema mbali na maoni ya wanachama, ofisi ya mwanasheria mkuu wa ACT Wazalendo imeagizwa kufanya rejea ya uzoefu wa nchi nyingine zenye mifano ya tume za uchaguzi zinazopigiwa mfano pamoja na ripoti na taarifa mbalimbali ikiwemo rasimu ya tume ya Jaji Joseph Warioba.

Katibu mkuu huyo aliwataka viongozi wa chama jimboni Nyasa kuwa chama kitaendelea kulipa kipaumbele suala la Tume Huru ya Uchaguzi ili chaguzi za mwaka 2024 (serikali za mitaa) na 2025 (Uchaguzi Mkuu) ziwe huru, za haki na zenye kuaminika.

Katibu Mkuu anaendelea na ziara yake mkoani Ruvuma na leo Jumatano, atakuwa jimbo la Songea Mjini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!