Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bulembo amshukia Polepole, ataka CCM amshughulikie
Habari za SiasaTangulizi

Bulembo amshukia Polepole, ataka CCM amshughulikie

Spread the love

MWENYEKITI Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi, Abdallah Bulembo amemmshukia mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole akimtaka kumwacha, mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan “amwache afanye majukumu yake kama Rais.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Bulembo aliyewahi kuwa mbunge wa kuteuliwa, amemwomba makamu mwenyekiti wa chama hicho-Bara, Philip Mangula kumchukulia hatua Polepole kwa matendo yake kama alivyowahi kuwahoji viongozi wengine wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Jumapili tarehe 12 Desemba 2021, amesema, “Lengo la Polepole ni kumkatisha tamaa Rais Samia. Hawezi ni mdogo sana. Rais Samia aachwe, namjua anaweza. Nimekaa naye namjua. Aachwe afanye kazi.”

Bulembo amesema, Polepole aliyewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, “najiuliza Mzee Philip Mangula yupo wapi kwa hili linaloendelea kwa Polepole? Kama aliweza kuwahoji makatibu wakuu Wazee Makamba na Kinana, ameshindwa nini kwa huyu Polepole? Mimi naamini, Polepole analo jambo na ukitaka kufanya jambo, usiseme nishikeni nisipigane, wewe pigana tu.”

3 Comments

  • Hahahaaa kale kativii chake anacho fundishia uongozi usio wanafunzi bila vyeti, wahuni tumesha kilamba tumembakishia takataka zake tuu pamoja na kunguni wake, hivisasa tv ipo ktk familia nyengine tunamtazama Jot Online tv. next?…

  • Kwa kweli inasikitisha watu wasio na nguvu ya hoja kutumia tabia hii kwa visasi.
    Afrika haiwezi kuendelea kwa wivu wa aina hii.
    Naomba Hamisi Mgeja na Abdallah Bulembo mtoe tafsiri yenu ya “wahuni.” Msimwingize Mama Samia kwenye haya malumbano yenu. Mama hahusiki.
    Nyerere aliwahi kusema, “kukosoa na kukosoana, ni silaha ya mapinduzi.” Sisi tunataka kujifunza kwa hoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!