January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtibwa Sugar yahitimisha dakika 630 za ukame

Spread the love

BAADA ya kucheza dakika 630 bila kuibuka washindi katika Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2021/22, hatimaye timu ya Mtibwa Sugar, imeonja radhi ya ushindi kwa kuitungua 2-0 Biashara United ya Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro…(endelea).

Ni ushindi wa kwanza kwa Mtibwa ikitumia uwanja wake wa nyumbani kwa mara ya kwanza tangu kuuacha kuutumia misimu mitatu iliyopita wa Manungu, mkoani Morogoro.

Ushindi huo ambao imeutapa Mtibwa, leo Jumapili tarehe 12 Desemba 2021, umewafanya kufikisha pointi tano kati ya michezo nane iliyocheza na kuwafanya kupanda nafasi moja kutoka mkiani hadi nafasi ya 15 juu ya Geita Gold Mine.

Katika michezo saba iliyocheza sawa na dakika 630, mitano ilifungwa na miwili kutoka sare.

Mtibwa ikicheza kandanda safi katika uwanja wake wa nyumbani, ilianza kuhesabu goli kwanza dakika ya 13 kwa kwaju wa penati, uliokwamishwa wavuni na Zingamasabo Styve.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza, zilimalizika kwa Mtibwa kwenda mapumziko na goli moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu.

Kiungo mkabaji, Said Hamis Ndemla, akipokea pasi safi nje, aliwazidi ujanja mabeki wa Biashara na kuachia mkwaju mkali na kwenda moja kwa moja wavuni na kuiandikia goli la pili ikiwa ni dakika ya 75.

error: Content is protected !!