Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Kitaifa Rais Samia afichua alivyokamatwa na polisi mara 3, aling’atwa mbu
Kitaifa

Rais Samia afichua alivyokamatwa na polisi mara 3, aling’atwa mbu

Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan amefichua namna alivyokamatwa na askari wa usalama barabarani mara tatu kwa makosa madogo ambayo yangetatulika bila kupoteza muda na kupelekwa kituo cha polisi licha ya kwamba alikuwa mkubwa serikalini. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Pia ameonya wataka askari wa usalama barabarani kuwa na lugha nzuri kwa raia na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Akizungumza leo tarehe 12 Desemba, 2021 wakati wa kufunga mafunzo ya kozi ya uofisa kutoka Chuo cha Maofisa wa Polisi Dar es salaam.

Katika mafunzo hayo, jumla ya maofisa ukaguzi 747 wamehitimu kozi hiyo na kupangiwa vituo vya kazi.

Rais Samia ametolea mfano namna alivyokamatwa askari wa usalama barabara kisha kupelekwa kituoni na kuwekwa kwa muda mrefu ahadi mbu wakaanza kumng’ata.

“Nilitaka kugongana na gari ya polisi… nikashika break. Wakatoka wakali wanafoka, mmoja akaingia kwenye gari yangu na wao na gari yao twende nakapelekwa. Nimefika naulizwa mwenye kosa nani, nikamwambia sijui mimi nimefikishwa hapa nadhani ndio mwenye kosa, saa nitafanyaje nikaandika statement.

“Nikaweka kwenye bao (benchi) kuanzia saa tisa au 10 nilipotoka kazini mpaka magharibi imeingia mbu wameanza kuingia. Najipiga hivi mbu wanauma naambiwa ‘mama acha wale tu hawana shamba hao’. Can you imaging nipo kituo cha polisi ndio lugha zenyewe hizo!.

Hata hivyo, amesema baadae bosi wa kituo hicho aliyemfahamu alitokea na kumuachia.

Amesema lugha nyingine za baadhi ya askari kwa raia hazipendezi ni za kibaguzi.

Pia Rais Samia ametolea mfano wakati alipofukuzwa na polisi alipokuwa akitoka harusini saa saba usiku baada ya kubainika kuwa taa moja ya gari yake haikuwa inawaka.

“Kweli nilipoangalia haiwaki, nikawaambia sawa itakuwa imeharibika njiani, niachie asubuhi nitarekebisha.

“Akaniambia sikuachii mmezidi nyie waarabu! akanipa makabila yote, tuende polisi, hapo tupo kilomita 15 nje ya kituo trafki cha polisi. Nikaendesha nikarudi tena usiku,” amesimulia.

Amesema alipofika kituoni baada ya kubainika ni Samia kwani kipindi hicho alikuwa mkubwa serikalini walimwachia lakini akawagomea kurudi mwenyewe usiku huo akapewa ulinzi hadi alipofika nyumbani kwaka umbali wa kilomita 20.

“Angeniachia asubuhi nikarekebisha ingekuwaje? Ni kutumia akili tu wakati mwingine!

Aliongeza kuwa mara nyingine askari anasimamisha anabishana, akiambiwa ingiza kichwa ndani ya gari tuzungumze anaingiza.

“Hebu fikiria askari polisi anaingiza bichwa lake ndani gari! hajui una nondo, nyundo.. ndio unatafuta vijisent unampa huyo anaondoka… jamani aliingiza kwangu nikamwambia nitakugonga nyundo akatoka mbio na mimi nikawasha gari nikaondoka.”

Amesema Jeshi la Polisi lina kazi nzuri za kufanya lakini bahati mbaya baadhi ya mambo hukiukwa.

Aidha, amemuagiza IGP Simon Sirro pamoja na wahitimu wa mafunzo hayo kwenda kuongea na wenzeo pamoja na kuwasimamia vizuri ili jeshi lisipate tuhuma kwa watu.

“Hiyo mifano niliyoitoa mimi imenifika, sikuwa mdogo, nilikuwa mkubwa mkubwa tu serikali, sasa hao raia wanyonge wa kawaida huko chini yanamfika yapi. Hayo ndio mambo ambayo yanashusha imani ya raia kwenye jeshi letu. Naomba mfanye marekebisho,” amesema.

1 Comment

  • Hongera Mama Samia!
    Polisi waonyeshe weledi wa kazi zao siyo usumbufu.
    Pale Morocco Road kwenda Mwananyamala kuna polisi wamevaa kiraia wanakamata watu wanapokata kona.
    Kibao kimewekwa kimakosa upande wa kulia badala ya kushoto. Mwendokasi upo kulia.
    Ndiyo, wakamatwe kwa sababu hawapo kazini. Wanatoa vitambulisho vya uongo. Wanakuchelewesha uendako utterly chochote. Aibu tupu kwa Polisi!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariKitaifa

Mabasi ya New Force yapigwa kitanzi kisa ajali

Spread the loveMAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imefuta ratiba za safari...

HabariKitaifa

Spika Tulia aeleza sababu za kengele ya hatari kulia Bungeni

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amesema kengele ya hatari...

HabariKitaifaTangulizi

Ni Bajeti ya kulipa madeni, mzigo wa kodi

Spread the love WAZIRI wa fedha, Mwigulu Nchemba, amewasilisha bajeti ya serikali...

Kitaifa

Serikali yatenga eka 10 kwa kila kijana mwenye sifa kufanya kilimo

Spread the love  SERIKALI nchini Tanzania imetenga eka 10 kwa kila kijana...

error: Content is protected !!