Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Aucho arejea, Yanga dimbani leo dhidi ya Mbeya kwanza
Michezo

Aucho arejea, Yanga dimbani leo dhidi ya Mbeya kwanza

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Yanga, hii leo itashuka dimbani kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya Kwanza huku kiungo wake mkabaji Khalid Aucho akirejea dimbani mara baada ya kukosa michezo miwili. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Sokoine Jijini Mbeya hii leo majira ya saa 1o jioni.

Aucho amerejea kikosini mara baada ya kukaa nje kutokana na kukabiliwa na majeraha katika siku za hivi karibuni, kabla ya kwenda kuitumikia timu yake ya Taifa ya Uganda kwenye michuano ya kuwania nafasi za kufuzu kombe la Dunia.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo huku ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1, kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo, uliofanyika kwenye dimba la Ilulu mkoani Lindi.

Mchezaji huyoa amekuwa na kiwango kizuri toka ajiunge na Yanga katika msimu huu wa mashindano akitokea nchini Misri na kuwa moja ya kivutio kwa mashabiki wengi wa timu hiyo na wapenda soka kiujumla.

Katika michezo sita waliocheza Yanga mpaka sasa, Aucho amekosa michezo miwili huku mmoja ukiwa dhidi ya Namungo FC, wakati Yanga ikiwa ugenini.

Kurejea kwa mchezaji huyo katika mchezo huu wa leo pengine utampa utayari kuelekea mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba, mchezo utakaopigwa Disemba 11, mwaka huu.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo huku ikiwa kileleni kwenuye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 16 huku ikifuatiwa na Simba kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 14.

Kwa upande wa Mbeya Kwanza ambao wamepanda Ligi kuu msimu huu, watavaana na Yanga kwa mara ya kwanza katika historia ya Timu yao toka kuanzishwa kwao.

Katika michezo sita waliocheza Mbeya Kwanza mpaka sasa imefanikiwa kuondoka na ushindi katika mchezo mmoja huku ikitoka sare mara nne na kupoteza mchezo mmoja

Mara baada ya mchezo huo Yanga itarejea jijini Dar es Salaam kujindaa na mchezo wa watani wa jadi, dhidi ya Simba ambao watakuwa wenyeji wa mchezo huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

error: Content is protected !!