January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Messi awabwaga, Lewandowski, Salah tuzo Ballon d’Or

Spread the love

 

MSHAMBULIAJI wa Psg na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi, ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or ya  mchezaji bora wa Dunia kwa mwaka 2021,mara baada ya kuwabwaga mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munchen Robert Lewandowski na Mohammed Salah ambaye anakip[iga kwenye klabu ya Liverpool. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika usiku wa kuamkia hii leo, Jijini Paris nchini Ufaransa.

Messi ameshinda tuzo hiyo na kuendelea kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyeshinda Ballon d’Or mara nyingi toka kuanzishwa kwa historia ya tuzo hiyo kubwa ulimwenguni inayotolewa na jarida moja la michezo nchini Ufaransa.

Mara baada ya kutwaa tuzo hiyo, Messi atakuwa amefikisja idadi ya Ballon d’Or saba, huku akifuatiwa na Cristiano Ronaldo ambaye ameshinda tuzo hiyo mara tano.

Katika msimu ulioamalizika Messi alifunga jumla ya mabao 41, na kutoa pasi za mabao 17 hukua kishinda mataji mawili ya Copa America akiwa na timu ya Taifa ya Argentina na Copa Del Rey akiwa na klabu yake ya zamani ya Barcelona.

Messi alianza kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2019 na kufanya hivyo mara tatu mfululizo mpaka 2012, kisha akaja tena kutwaa mwaka 2015, 2019 na 2021.

 

error: Content is protected !!