January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizara ya ulinzi yajipanga kumaliza migogoro ya ardhi, kulipa fidia

Spread the love

 

WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa amesema ipo katika mchakato wa kupima maeneo 96 ili kutatua migogoro ya ardhi iliyopo baina ya wananchi na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo. Anaripoti Danson Kaijage – Dodoma… (endelea)

Hayo yamebainishwa jana tarehe 29 Novemba, 2021 jijini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Stergomena Tax wakati akitoa taarifa ya mafanikio na changamoto za wizara hiyo kwa kipindi cha miaka 60 tangu Uhuru wa Tanzania bara ulipopatikana.

Pia Tax amesema wanaendelea kufanya tathmini ili kubaini kiasi cha madeni ya fidia ili kuwalipa fidia wale wote ambao watastahili kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria.

Amesema hadi sasa tayari maeneo zaidi ya 56 yamekwishapimwa.

Pamoja na mambo mengine amesema katika kipindi cha miaka 60, Tanzania imefanikiwa kulinda mipaka yake pamoja na kushinda vita vya Kagera ambayo ilirejesha eneo la Kagera ambalo lilikuwa linachukuliwa na Nduli Iddi Amini Dada.

“Baadhi ya majukumu wizara kupitia JWTZ imeendeleza jukumu lake la kulinda mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhakikisha mipaka ya nchi yetu ambayo inajumuhisha eneo la nchi kavu, anga na la maji inandelea kuwa salama.

“Kwa ujumla hali ya mipaka baina ya nchi yetu na nchi jirani imeendelea kuwa salama” amesema Waziri.

error: Content is protected !!