Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe: Hatima pingamizi la Serikali J3
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe: Hatima pingamizi la Serikali J3

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mawasiliano jijini Dar es Salaam, imepanga kutoa uamuzi wa pingamizi la Jamhuri ya kupinga kupokelewa kwa barua iliyowasilishwa na mahakamani hapo na Mohamed Abdillah Ling’wenya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ling’wenya ambaye ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo ya ugaidi inayomkabili yeye pamoja na wenzake watatu akiwemo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Adam Kasekwa na Halfan Bwire.

Kwa pamoja, wanatuhumiwa kupanga njama za vitendo vya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kulipua vituo vya mafuta na kudhuru viongozi wa serikali.

Pingamizi hilo, liliwekwa jana Alhamisi, tarehe 25 Novemba 2021, wakipinga barua hiyo iliyoandikwa na mawakili wa utetezi kwenda kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar es Salaam ili kumuomba baadhi ya nyaraka kwa ajili ya kuitumia katika kesi yake ndogo.

Barua hiyo ilikuwa na lengo la kumuomba baadhi ya nyaraka kwa ajili ya kuitumia katika kesi yake ndogo. Nyaraka hizo ni, stationary diary ambacho ni kitabu kinachoonesha maudhurio ya askari polisi na kitabu kinachoonesha matukio yaliyotendeka katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar ea Salaam, 7 Agosti mwaka huu.

Baada ya mawakili wa pande zote kutoa hoja zao za kupinga na ama kutetea, Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo, amepanga kutoa uamuzi saa 3:00 asubuhi ya Jumatatu, tarehe 29 Novemba 2021.

“Basi tunaihairisha shauri hili mpaka tarehe 29 Novemba 2021, saa 3 asubuhi na shahidi utaendelea kuja kutoa ushaidi wako siku hiyo baada ya mahakama kutoa maamuzi,” amesema Jaji Tiganga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!