January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kina Mbowe wamtega Jaji Tiganga

Spread the love

 

MAWAKILI wa utetezi, katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ba wenzake, wameiomba Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, ipokee barua yao kwa ajili ya kielelezo katika kesi yao ndogo,  kama ilivyopolea barua ya upande wa mashtaka. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ombi hilo limetolewa na mawakili hao, leo Ijumaa, tarehe 26 Novemba 2021, wakati wanawasilisha hoja zao dhidi ya mapingamizi ya upande wa mashtaka, kupinga barua iliyoandikwa na utetezi kwenda kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar es Salaam, isipokelewe kama kielelezo cha ushahidi wa mshtakiwa wa tatu, Mohamed Abdillah Ling’wenya.

Jana Ling’wenya aliomba mahakama ipokee barua hiyo, aliyoelekeza mawakili wake waiandike ili kumuomba RPC Ilala nyaraka kuthibitisha ama kutothibitisha shahidi wa pili wa jamhuri, Askari Mpelelezi Msemwa, alimpokea mshtakiwa huyo na mwenzake, Adam Kasekwa, katika mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, tarehe 7 Agosti 2020.

Wakili wa mshtakiwa huyo wa tatu, Dickson Matata ameiomba mahakama hiyo irejee maamuzi yake iliyotoa dhidi ya mapingamizi yao kuhusu barua ambayo ilikuwa kielelezo cha jamhuri, inayomthibitisha Askari Msemwa, alikipokea kitabu cha mahabusu (DR) cha kituo hicho, kutoka kwa Naibu Msajili wa Mahakama hiyo.

“Wakati mahakama inatoa uamuzi ijikumbushe maamuzi iliyotoa mwezi mmoja ulipoita ambayo imetoa tarehe 16 Novemba 2021, ambapo ilisema wakati wa kuipokea barua iliyoletwa na shahidi wa pili wa jamhuri kwenye trial  with in trial,  Askari Msemwa ambayo ilikuwa imetoka kwa naibu msajili wa mahakama hii kwenda,  kwa Ofisi ya Mashtaka Dodoma. Amnayo ilikuwa copy kwa Askari Msemwa kama ambavyo barua hii imekuwa copied kwa shahidi aliyepo kizimbani,” amedai Wakili Matata.

Wakili Matata amedai “mahakama ilitoa uamuzi kwamba mtu akiwa copied inakiwa na pressumption kwamba ameipokea.”

Naye Wakili John Mallya, amemuomba Jaji Tiganga itumie uamuzi wa shauri hilo dogo katika kutoa maamuzi dhidi ya kupokelewa kwa barua hiyo ya utetezk.

“Mahakama hii ina bahati kukutana na mazingira kama haya kwenye shauri hilihili wakati wa kupokelewa kielezo namba moja. Mahakama iangalie ile ilichokiamua kwenye kupokea kidhibiti kile. Kwa ufahamu wangu vidhibiti vinafanana naomba mahakama ikipokee,” amedia Wakili Mallya.

Mawakili wa jamhuri waliweka pingamizi dhidi ya barua ya utetezi wakidai kukosekana kwa uwezo au kuaminika kwa nyaraka hiyo na shahidi aliyetaka kuitoa. Pia walidai  barua hiyo haina umuhimu, vilevile shahidi huyo hakujenga msingi wa kukitoa.

Mnamo tarehe 15 Novemba 2021, mahakama hiyo ilitupa pingamizi la utetezi dhisi ya kupoklea barua ya upande wa mashtaka kama kielezo namba moja, na kuiopokea barua hiyo.

Ambapo Jaji Tiganga alisema ameipokea barua hiyo kwa kuwa ni muhimu na kwamba mawakili wa utetezi watapima uwezo wake na wa shahidi aliyeitoa wakatu wa maswali ya dososo.

Jaji Tiganga alisema, Sheria ya Ushahidi inaruhusu shahidi kuaminika na au kuwa na uwezo kupitia ushahidi wake.

Mbali na ombi hilo kwa Jaji Tiganga, Wakili Matata alitoa hoja nyingine dhisi ya pingamizi hilo, Wakili Matata aliomba mahakama hiyo itupilie mbali pingamizi hilo, akidai kuwa, Wakili wa Serikali wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula, wakati akiwasilisha hoja zake alishindwa kuisaidia mahakama hiyo.

Kwa kutotaja  Amri za Magereza  (Prison General Orders), zinazomnyima uhuru mahabusu au mtuhumiwa kwa kuwa yuko chini ya ulinzi wa Jeshi la Magereza. Na kwamba chochote kitakachofanyika dhidi yake kithibitishwe na Mkuu wa Magereza.

Wakili Matata alidai kuwa, ni wasilisho lao kuwa amri hiyo haipo na hivyo pingamizi lao halina nguvu kisheria “ni wasilisho letu kwamba uhusiano baina ya wakili na mteja wake ni previlage (upendeleo) na unalindwa na sheria na katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Ibara ya 13,  ibara ndogo 6B ya katiba yetu  ya 1977, kama ambavyo imefanyiwa marejeo mara kwa mara.”

“Kwa kuzingatia haki hii, sisi mawakili tulikuwa na haki sio tu ya unapokuwa mahakamani lakini pia hata tunapoenda gerezani tunaruhusiwa kuonana na wateja wetu siku yoyote. Ukisoma prison general orders ambazo kimsingi mheshimiwa jaji orders hizi zimelenga kucontrol uhusiano baina ya askari magereza wenyewe namna wanavyofanya shughuli zao,  lakini pia baina ya askari magereza na watuhumiwa ama wafungwa,” amedai Wakili Matata.

Wakili Matata aliendelea kudai “utaratibu ulioko magereza ambao unahusisha bwana jela kuhusishwa na mhuri kugongwa ni wa namna moja, aidha pale mtuhumiwa au mahabusu akiwa ndani ya gereza anapotaka kuandika barua kwenda nje, mahakamani au kwa wakili wake ndipo mtahitaji barua ya bwana jela na mhuri wa magereza,”

“Namna ya pili ni mtu anapotoka nje mfano wakili na ananyaraka anataka mtuhumiwa kwenda kuisaini hapo bwana jela atahusishwa na kitakachofanyika wataichukua hiyo nyaraka wataitype wao wakishaitype kwa coment zilezile wataipeleka ataisaini mtuhumiwa na kisha wataigonga mhuri kisha wakili utakabidhiwa na kuondoka nayo.”

Aidha, Wakili Matata alidai, wakati akitoa ushahidi wake,  shahidi huyo alidai  alioneshwa  barua na wakili wake akiwepo Wakili Kibatala, na kuwa hakukaa nayo muda wote bali alioneshwa tu.

“Jaji kwa kusema alionyeshwa hapa mahakamani hoja ya kuwa barua ile iltakiwa kuwa na mhuri wa magereza na kupitia kwa bwana jela inakosa mashiko

Ni wasilisho letu pia kwamba, mteja anapokuwa kwenye eneo la mahakama anakuwa na haki ya kuonana na mawakili wake na kuwasiliana na watu, kinachotakiwa ni kuwaomba askari magereza kupitia kiongozi wao wa siku hiyo na kuweza kuwasiliaan na mteja wako,”

Kuhusu hoja ya jamhuri iliyodai shahidi huyo hana uelewa dhidi ya barua hiyo kwa kushindwa kutamka kwa ufasaha jina la Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi, lililoandikwa katika muhuri uliopigwa katika barua hiyo, Wakili Matata ameijibu akidai hawakupata muda mzuri wa kumuandaa shahidi.

“Jaji napenda niikumbushe mahakama kwamba jana tulikuwa tunajua upande wa jamhuri unakuja kuendelea na ushahidi lakini wakaja na kufunga ushahidi wao. Tunajiuliza angewezaje shahidi kutoa ushahidi wake kama hatujapata nafasi ya kukaa naye na kumuandaa kwa ajili ya kutoa ushahidi na kama hiyo ilifanyika chini ya uangalizi wa askari magereza ambao kimsingi inaruhusiwa. Kuna kosa gani shahidi kuoneshwa barua ambayo yeye mwenyewe alikuwa muelekezaji wa barua hiyo kuandikwa? Kupitia wakili wake Fredy akiwa pamoja na wakili kiongozi wa jopo la utetezi,” alidai Wakili Matata.

Wakili Matata alidai”aliweza kuonesha unique fitures za barua hiyo na akasema kwenye hizi unique fiture ina kesi namba 16 ya 2021, hakuishia hapo akasema kuna jina na sahihi ya wakili kiongozi  Peter Kibatala. Akasema pia kwenye barua hiyo kuna jina la Msemwa ambayo alikuwa shahidi namba mbili kwenye trial with in trial akasema pia kuna mhuri wa mahakama  japo alikuwa ansema mahakama kuu divisheni na neonmahakama kuu divisheni iko kwenye mhuri.”

Pia, Wakili Matata alidai kwamba, shahidi huyo ana uelewa kuhusu barua hiyo akidai kuwa, katika ushahidi wake alieleza mahakama  kuwa anatambua saini ya Wakili kibatala, akidai alikuwa anawatetea tangu katika hatua ya usikilizwaji mwenendo wa mashtaka. Pia aliitambua kwa kutaja baadhi ya maudhui yanayodaiwa kuwemo ndani ya barua hiyo.

Katika hoja ya jamhuri iliyodai kuwa shahidi siyo wa kuaminika, Wakili Matata aliijibu akidai “jaji tukija kwenye suala la competence ni submission yetu kwamba shahidi pamoja na barua aliyotaka kuitoa ni competent, hii inatokana na ukweli kwamba shahidi yeye ndiye aliyeanzisha au aliyetoa maelekezo kwa Wakili Fredy,  pamoja na Wakili Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi,  Peter Kibatala.”

Wakili Matata aliijibu hoja ya jamhuri kuhusu barua hiyo kutokuwa na umuhimu, akidai  wakati Ling’wenya anayoa ushahidi wake, alieleza namna ilivyo muhimu akisema ililenga kumuomba RPC Ilala nyaraka hizo, ili kuthibitisha ama kitothibitisha ushahidi alioitoa Askari Msemwa, akidai aliwapokea kituoni hapo tarehe 7 Agosti 2020, wakati wao wanakana hawakuwahi kifikishwa.

“Ling’wenya alitoa maelekezo ya barua kuandikwa kwenda kwa RPC wa Ilala akasema lengo la barua ile ni kutaka kupata vitu vitatu ambavyo alivitaja kwamba apate movement order ya huyo Askari Msemwa ambayo inaonesha alivyotoka Central Polisi Dar es Salaam na kupelekwa Oysterbay,  pili akasema alitaka apatiwe OB  ambayo aliisema ni kitabu kinachoandikwa matukio ya siku hiyo,  lakini pia akazungumzia station diary ambayo yeye anaiita stationery diary ambayo alifafanua akitumia kifaa cha jeshini kwao akasema inaonesha askari ulitoka saa ngapi,  umeingia saa ngapi kama umepewa silaha inaonesha,” alidai Wakili Matata.

Naye Wakili Kihwelo alidai Ling’wenya alieleza namna alivyotoa maelekezo ya uandikwaji wa barua hiyo, ns kuwa   lengo ni kutaka kuitoa barua hiyo ni mtu ajue na pia mshtakiwa huyo alikuwa na haki ya kuitumia.

Wakili Kihwelo alidai kuwa, shahidi huyo alijenga msingi wa mnyororo wa utunzwaji wa kielelezo hicho hadi kumfikia kwake .

“Kwa msingi huo ni wasilisho letu kwamba, shahidi alijenga msingi na muda wote ambao ametoa ushahidi mahakanani hapa ametoa ushaidi ambao ana taarifa nao lakini pia ushahidi anaoufahamu,” alidai Wakili Kihwelo.

Baada ya upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao, Jamhuri kupitia Wakili Chavula alitoa hoja kinzani, akidai kwamba hoja zao hazikugusa misingi ya mapingamizi yao.

“Tumesikia hoja kinzani za wenzetu kina Matata na Kihwelo na kimsingi ni hoja yetu kwamba hoja hizi zote walizozitoa hazijagusa misingi ya hoja zetu, isipokuwa hoja hizi zimekuja kutia nguvu misingi ya hoja zetu ,” alidai Wakili Chavula.

“Walitakwia waende mbali zaidi wakati wanamuongoza shahidi, aeleze ufahamu wake wa yaliyomo humo ndani ambalo hilo hawakulifanya. Katika submission zake Matata walikuwa wanasisitiza mahakama kuwa, walikuwa wanamuonesha kielelezo,” alidai Wakili Chavula na kuongeza:

“Hakuna sehemu walionesha na wakamuongoza shahidi wao kusema alikuwa anakimiliki kwa hiyo hata misingi ya hili pingamizi wameshindwa kuikidhi.

Ni maoni yetu kwamba hoja yao kwamba waliweza kujenga uwezo wa shahidi haina mashiko.

error: Content is protected !!