Tuesday , 30 April 2024
Home Kitengo Michezo Maandalizi mkutano mkuu Simba yakamalika
MichezoTangulizi

Maandalizi mkutano mkuu Simba yakamalika

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba inatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka wa wanachama, huku sehemu kubwa ya shughuli hiyo ikiwa imeshakamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mkutano huo utafanyika Jumapili ya tarehe 21, Novemba 2021, kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.

Akizungumza kuelekea mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki Hamisi Kissiwa, amesema kuwa kuwa mkutano huo unatarajia kuanza majira ya saa 3 asubuhi na kuwakumbusha wanachama wa klabu hiyo kulipa mapema ada zao ili kuepuka usumbufu na kuweza kuwa sehemu ya tukio hilo.

“Mkutano unatazamiwa kuanza saa 3 asubuhi na tunatazamia kumaliza mapema kwa hali ilivyo na ajenda zilivyo.”

“Ili uweze kuingia kwenye mkutano, lazima ulipie ada yako na uasiwe na madeni, njoo na kadi yako ili siku ya jumapili uingie salama bila shida yoyote.” Alisema Kissiwa

Mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa ibara ya 21 (1), ya katiba ya klabu hiyo ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2016, kwa kuruhusu mfumo wa mabadiliko ya uwendeshaji wa klabu hiyo.

Mara ya mwisho Simba kufanya mkutano mkuu wa mwaka, ilikuwa tarehe 7 Februari 2021, ambapo moja ya ajenda ilikuwa kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi ya mwenyekiti na Murtaza Mangungu alifanikiwa kushinda nafasio hiyo iliyoacha wazi na Swedy Nkwabi ambaye alijiuzuru.

Mangungu alishinda kiti hiko mara baada ya kumshinda mpinzani wake, Juma Nkamia kwa kupata kura 802, kati ya kura 1140 zilizopigwa na wanachama waliojitokeza kwenye mkutano huo.

1 Comment

  • Duh!
    Mnafanya uchaguzi bila kuwa na robo tatu ya wanachama?
    Je, ile kampuni iliyoingia ubia na Simba si imempa Mo time nzima. Kama Mo anaipenda Simba, si angeweka lebo ya Mohammed Enterprise kwenye jezi za Simba na kuipa klabu hela kama Etihad na Emirate?
    Matajiri wanaokwenda Simba au Yanga hawainui mpira…wanafuata pesa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari za SiasaTangulizi

Wizara Katiba na Sheria yaliomba Bunge Sh. 441.2 bilioni

Spread the love  WIZARA ya Katiba na Sheria imeliomba Bunge liidhinishe bajeti...

error: Content is protected !!