SAMAKI ni kitoweo pendwa kwa watu wengi duniani, hususani wakazi wa maeneo ya pwani na kando ya mito na maziwa. Lakini kwa wakazi wa Lamu nchini Kenya, samaki aina ya taa ni hatari pale anapokung’ata anasababisha usishiriki tendo la ndoa na mkeo kwa muda wa miezi sita. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)
Hali hiyo imeibua hofu kwa wanaume wakazi wa Kaunti hiyo la Lamu kwa sababu ni tisho kubwa kwa maisha yao na ya kifamilia.
Samaki huyo aina ya taa ni mkubwa na mwenye umbo bapa na mkia mrefu ambao ncha yake ina maumbile kama ukucha unaoaminika kuwa na sumu kali.
Wakazi wa Lamu wanaamini anayedungwa na taa hastahili kushiriki mapenzi na mkewe kwa karibu miezi sita wakati akiuguza kidonda.
Mzee wa kisiwa cha Kizingitini, Khaldun Vae amewaeleza waandishi wa habari nchini humo kuwa imani hiyo imekita mizizi tangu enzi za mababu katika vijiji vyao.
“Baadhi ya ndoa zimekuwa zikiyumba punde waume wanapojeruhiwa na samaki huyo.
“Tangu enzi za mababu zetu, huwezi kudungwa na mwiba wa taa na kabla hujapona unakimbilia kulala na mkeo. Huko ni kujichimbia kaburi,” alisema Vae.
Leave a comment