Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo DR Congo yasonga mbele, Stars yabanwa Madagascar
Michezo

DR Congo yasonga mbele, Stars yabanwa Madagascar

Spread the love

 

MICHEZO ya kundi J kuwania kufuzu kombe la dunia Qatar 2022, imemalizika kwa timu ya DR Congo kusonga hatua inayofuata huku Taifa Stars ya Tanzania ikibanwa mbavu na Madagascar kwa kutoka 1-1. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

DR Congo imesonga mbele hatua inayofuata, baada ya kuitandika Benin 2-0, katika uwanja wake wa nyumbani na kuwafanya kuongoza Kundi J kwa kufikisha pointi 11 huku Benin ambayo awali ilikuwa ikiongoza kundi hilo, ikisalia na pointi zake 10.

Katika mchezo mwingine wa kuhitimisha kundi hilo, imeshuhudia timu ya Tanzania ya Taifa Stars ikiwa ugenini ikilazimishwa sare wa 1-1 dhidi ya Madagascar.

Sare hiyo imewafanya Stars kusalia nafasi ya tatu ikiwa na pointi nane huku Madagascar ikimaliza michuano hiyo ikishika mkia kwa pointi nne.

Bao hilo la Stars limewekwa kimiani na dakika ya 25 kipindi cha kwanza na Saimon Msuva akiunganisha pasi safi ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ huku Madagascar ikisawazisha dakika ya 74 na Hakim Abdallah.

1 Comment

  • Soka limeporomoka….ni album tupu! TFF ya Karia yenye rushwa ilaumiwe 60%. Wabunge 40%. Ndiyo, wabunge hamjatunga sheria inayolinda vilabu vya wanachama kama ilivyo Ujerumani, Brazil, n.k.
    Ningependa kuona maBakhresa wengi kuliko maMoDewji na maManji wanaovinyonya vilabu vikubwa nchini. Kama kweli wanataka kuendeleza soka, wanzishe vilabu vyao.
    Tuache kudanganyana karne ya 21.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

error: Content is protected !!