November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

DR Congo yasonga mbele, Stars yabanwa Madagascar

Spread the love

 

MICHEZO ya kundi J kuwania kufuzu kombe la dunia Qatar 2022, imemalizika kwa timu ya DR Congo kusonga hatua inayofuata huku Taifa Stars ya Tanzania ikibanwa mbavu na Madagascar kwa kutoka 1-1. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

DR Congo imesonga mbele hatua inayofuata, baada ya kuitandika Benin 2-0, katika uwanja wake wa nyumbani na kuwafanya kuongoza Kundi J kwa kufikisha pointi 11 huku Benin ambayo awali ilikuwa ikiongoza kundi hilo, ikisalia na pointi zake 10.

Katika mchezo mwingine wa kuhitimisha kundi hilo, imeshuhudia timu ya Tanzania ya Taifa Stars ikiwa ugenini ikilazimishwa sare wa 1-1 dhidi ya Madagascar.

Sare hiyo imewafanya Stars kusalia nafasi ya tatu ikiwa na pointi nane huku Madagascar ikimaliza michuano hiyo ikishika mkia kwa pointi nne.

Bao hilo la Stars limewekwa kimiani na dakika ya 25 kipindi cha kwanza na Saimon Msuva akiunganisha pasi safi ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ huku Madagascar ikisawazisha dakika ya 74 na Hakim Abdallah.

error: Content is protected !!