Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Majaliwa ataka wadau kuwekeza soka la vijana
Michezo

Majaliwa ataka wadau kuwekeza soka la vijana

Spread the love

 

KUFUATIA kipigo cha mabao 3-0, walichokipata timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Congo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wadau, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kuwekeza kwenye soka la vijana ili kupata wachezaji watakaounda timu ya taifa imara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Majaliwa ameyasema hayo leo tarehe 12 Novemba 2021Jijini Dodoma kwenye hotuba yake ya kuahirisha mkutano wa tano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hadi Jumanne Februari Mosi, 2022, saa 3 asubuhi.

Katika hotuba yake Waziri Mkuu alisema kuwa matokeo hayo mabaya kwa Taifa Stars waliyoyapata dhidi ya Jamhuri ya Congo wadau wa soka watumie kujitasmini na kuja na mikakati bora ili kuweza kufanya viozuri huko mbeleni.

“Uongozi wa Tff, benchi la ufundi na wadau wa soka tutumie matokeo ya jana  kujitasmini na kuja na mkakakati bora wa kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.” Alisema Majaliwa

Mchezo huo wa kundi J, Taifa Stars dhidi ya Congo ulipigwa Alhamisi Novemba 11, Mwaka huu kwenye dimba la Benjamin Mkapa, huku Waziri akiwa ndio mgeni rasmi kwenye mechi hiyo.

Aidha Majaliwa aliendelea kwa kusisitiza kuwa, kuna haja ya kuwekeza kwenye soka la vijana na kuboresha Ligi ya ndani ili kuweza kupata wachezaji bora watakaoweza kuunda timu ya Taifa imara.

 “Tuendelee kuwekeza kwa vijana wetu, tuboreshe Ligi yetu, tuimalishe klabu zetu ili tuweze kupata wachezaji bora watakaoweza kuunda timu ya taifa na kushindana na wenzetu kwenye medani ya kimataifa.” Alisisitiza Waziri Mkuu

Wakati kiongozi huyo ambaye pia ni msimamizi wa shughuli za Serikali Bungeni akiongea hayo, muda mchache baadae  Taifa Stars itaanza safari ya  kuelekea nchini Madagascar kwa ndege maalumu kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba kundi J, dhidi ya wenyeji hao.

Msafara wa Taifa Stars utaondoka ukiwa na wachezaji 27, ambao waliingia kambini toka Novemba 4, Mwaka huu chini ya kocha Kim Poulsena na kufanya maandalizi ya michezo hii miwili.

Ndoto ya Stars kufuzu kwa hatau inayofuata, ilizimwa rasmi mara baada ya Timu ya Taifa ya Benin kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, kwenye mchezo wake dhidi ya Madagascar na kufanya kufikisha pointi 10 na kusalia na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Congo.

Mchezo huo wa mwisho kati ya Jamhuri ya Congo na Benin, utakaopigwa Jumapili tarehe 14, Novemba 2021 jijini Lubumbashi kwenye Uwanja wa TP Mazembe ndio utakaotoa kinara wa kundi hilo ambaye atafuzu kwa hatua inayofuata ya mtoani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!