November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sarah, Tuchel watamba Tuzo EPL

Spread the love

 

MSHAMBULIJI wa klabu ya Liverpool Mohammed Sarah ameshinda tuzo ya mchezo bora mwezi Oktoba, huku kocha Mkuu wa Chelsea akitwaa tuzo ya kocha bora mwezi huo huo, kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Sarah ameshinda tuzo hiyo mara baada ya kuwashinda mlinda mlango wa Arsenal Aaron Ramsdale, winga wa Burnley Maxwel Cornet, beki wa kati wa Southampton Tino Libramento na mchezaji wa Leicester City Youri Tielemans.

Ndani ya mwezi Sarah mwenye umri wa miaka 29, amefunga jumla ya mabao matano akiwa na timu yake ya Liverpool, huku mabao matatu (hat trick) akifunga kwenye mchezo mmoja dhidi ya Manchester United, ambao ulimalizika kwa Liverpool kushinda mabao 5-0.

Mara ya mwisho Sarah kushinda tuzo hiyo, ilikuwa machi 2018, akiwa bado mchezaji wa Liverpool.

Kwa upande wa kocha wa Chelsea Thomas Tuchel aliibuka kinara wa tuzo hiyo mbele ya kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, kocha wa West Ham David Moyes na Patrick Vieira anayekinoa kikosi cha Crystal Palace.

Ndani ya mwezi Oktoba Tuchel ameiongoza Chelsea ambao ndio vinara wa Ligi kwenye michezo minne, na kuibuka na ushindi kwenye michezo yote, huku safu yake ya ushambuliaji ikifunga mabao 14.

Katika michezo hiyo minne ambaye kocha huyo ameiongoza Chelsea, michezo mitatu timu yake haijaruhusu bao hata moja.

 

 

error: Content is protected !!