Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko 12 waibuka washindi NMB bonge la Mpango
Habari Mchanganyiko

12 waibuka washindi NMB bonge la Mpango

Spread the love

 

NAKAUNDA Mangosongo na Charles Mkwizu ambao ni wakazi wa Dodoma wamejishindia pikipiki za miguu mitatu aina ya Sky Mark katika droo ya kwanza ‘NMB Bonge la Mpango – 2merudi Tena.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Droo hiyo ilichezeshwa jana Jumatano, tarehe 13 Machi 2021 ya shindano hilo awamu ya pili ya kampeni ya weka akiba na ushinde inayoendeshwa na benki hiyo.

Mbali na Mangosongo na Mkwizu, washindi wengine 10 waliojinyakulia fedha taslimu Sh.100,000 ni: Kuluthum Chande, George Fabiano, Justine Yona, Justina Mbuya na Beatrice Tarimo.

Pia, wamo Gloriana Nicholaus, Paschal Phabian, Alphonce Donatus, Ramadhani Khalfan, Kelvin Mosha.

Akizungumza kabla ya kuchezeshwa kwa droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite, alisema katika kipindi chote cha kampeni hiyo ya wiki 12, zawadi zote zenye thamani ya Sh.237 milioni zitaenda kwa washindi 170, ambao wataweka akiba katika akaunti ama kufungua akaunti mpya zenye akiba isiyopungua Sh.100,000.

“Kila wiki tutakuwa na droo za kupata washindi 12, wakiwemo 10 wa pesa taslimu Sh.100,0000 kila mmoja huku wengine wawili wakijishindia pikipiki za miguu mitatu (moja kwa kila mmoja), aina ya Sky Mark yenye thamani ya Sh.4.5 milioni.”

Ngingite aliwaomba wateja wa benki hiyo kuendelea kujiwekea akiba ili kujiongezea nafasi ya kushinda fedha taslimu ama pikipiki.

“Na kwa wale wasio na akaunti, watembelee matawi yetu yaliyotapakaa kote nchini, waweze kufungua akaunti na kuweka akiba angalau ya Sh laki moja, waingie kwenye droo hizi na kushinda,” alisema Ngingite.

Droo hiyo ilichezeshwa mbele ya afisa toka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT), Joram Mtafya, ambaye aliwahakikishia Watanzania kuwa kampeni hiyo itafanyika kwa kufuata sheria na kanuni zinazosimamia michezo hiyo na kwamba, hata akaunti za watoto walio chini ya umri wa miaka 18 (zinazoendeshwa na wazazi ama walezi), zinaweza kushinda zawadi hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!