October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aweka shada la maua kaburi Hayati Magufuli

Rais Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la Hayari John Magufuli

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameweka shada la maua kaburi la aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Hayati John Pombe Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Ni leo Alhamisi, tarehe 14 Oktoba 2021, nyumbani kwa Hayati Magufuli, Chato mkoani Geita.

Rais Samia amefika nyumbani kwa Hayati Magufuli akiwa njiani kwenda Uwanja wa Magufuli, kuhudhuria kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2021.

Magufuli, alifikwa na mauti saa 12 jioni ya tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, iliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam na mwili wake, kuzikwa 26 Machi 2021.

Mara baada ya kifo hicho, Samia aliyekuwa Makamu wa Rais, aliapishwa kuwa Rais tarehe 19 Machi 2021.

error: Content is protected !!