Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sabaya na wenzake kusuka, kunyoa kesho
Habari za Siasa

Sabaya na wenzake kusuka, kunyoa kesho

Lengai Ole Sabaya akiwa mahakamani Arusha
Spread the love

 

HUKUMU ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili itaolewa kesho Ijumaa tarehe 15 Oktoba, 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Ni baada ya kuahirishwa kutolewa mahakamani hapo, tarehe 1 Oktoba 2021.

Mbali na Sabaya, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, ambao wanadaiwa kuvamia na kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha wa zaidi ya Sh. 2.7 milioni, katika duka la Mohamed Saad, tarehe 9 Februari 2021.

Shahidi wa mwisho upande wa utetezi, ambaye alitoa ushahidi wake, alikuwa ni Mbura, akiongozwa na jopo la mawakili wa utetezi, likiongozwa na Wakili Dancan Oola.

Baada ya ushahidi huo kufungwa, Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, aliiomba mahakama hiyo itoe siku saba kwa pande zote mbili, kuwasilisha majumuisho ya kesi hiyo kwa njia ya maandishi.

Hakimu Amworo alikubali ombi hilo na kutoa siku saba kwa pande zote mbili, kuwasilisha majumuisho hayo.

Kesi hiyo, ilisikilizwa mfululizo kuanzia tarehe 19 Julai hadi 24 Agosti 2021. Ni baada ya Sabaya na wenzake, kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo mhakamani hapo, tarehe 16 Julai 2021.

Aidha, tarehe 24 Agosti 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo alipanga tarehe 1 Oktoba kuwa siku ya hukumu baada ya mahakama hiyo kumaliza kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili.

Sabaya alifikishwa mahakamani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kumsimamisha tarehe 13 Mei 2021 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili.

Sabaya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha, anza safari ya kuwa mkuu wa wilaya ya Hai, tarehe 28 Julai 2018 na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!