Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ripoti haki za binadamu Tanzania yatinga UN, kujadiliwa Novemba 5
Habari Mchanganyiko

Ripoti haki za binadamu Tanzania yatinga UN, kujadiliwa Novemba 5

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imewasilisha ripoti ya utekelezwaji wa haki za binadamu (UPR), katika kipindi cha miaka minne mfululizo (2016-2020), katika Baraza la Haki za Binadamu, la Umoja wa Mataifa (UNHRC), kwa ajili ya kujadiliwa tarehe 5 Novemba 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 5 Oktoba 2021 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju, akifungua kikao cha maandalizi ya wadau wa haki za binadamu, kuhusu ujadiliwaji na upitishwaji wa taarifa hiyo, inayotarajiwa kujadiliwa Geneva nchini Uswisi.

Kikao hicho kimeandaliwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), yanayotetea haki za binadamu nchini, ikiwemo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

“ Hiki ni kikao cha maandalizi kuelekea ujadiliwaji na upitishwaji wa taarifa yetu ya nchi, ambayo tumeiwasilisha tarehe 9 Agosti 2021, kuhusu namna tulivyotekeleza masuala ya haki za binadamu ndani ya miaka minne,” amesema Mpanju.

Mpanju amesema, taarifa hiyo imewekwa katika mtandao wa UNHRC, na kwamba itajadiliwa tarehe 5 Novemba mwaka huu, ambapo Serikali ya Tanzania itatuma wawakilishi wake kujibu hoja zitakazoibuliwa.

“Tunahimiza nchi zote za UN zitakazoshiriki kwenye kujadili taarifa ya nchi, kutoa mapendekezo yaliyowazi, yanayoeleweka na kuzingatia sheria na katiba ya nchi yetu,” amesema Mpanju.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Katiba na Sheria, amesema mzunguko uliopita Serikali ilikataa mapendekezo 94 kati ya 227, kwa kuwa yalikuwa kinyume na sheria, katiba na mila za nchi.

Naye Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema lengo la kikao hicho ni kujadili UPR ili kutoa mapendekezo yao, kabla haijajadiliwa na UNHRC.

“UPR ni mchakato wa kila baada ya miaka minne, ambao uko chini ya UN, walikubaliana kila baada ya miaka minne Taifa linapitiwa kuhusu utekelezwaji wa haki za binadamu,”

“ 2016 tulipata mpendekezo 230, Tanzania ikakubali 133, sasa tunachofanya kuangalia hayo 133 imeweza kutekeleza mangapi, lakini tunatoa mapendekezo mengine kwa ajili ya mapitio mengine ambayo yanafanyika mwaka huu,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema, katika kipindi cha miaka minne, Tanzania imefanya vibaya katika masuala ya uhuru wa kujieleza na taasisi za watetezi wa haki za binadamu.

“Kwa miaka minne haki za binadamu hazikwenda vizuri kwa maoni yetu, ndiyo maana sisi tuna ripoti yetu na Serikali ina ya kwao na sisi tuna uhuru wa kuandika tulichokiona,” amesema Olengurumwa na kuongeza:

“Tumesema kuna maeneo tumefanya vizuri na kuna maeneo tumefanya vibaya, mfano uhuru wa kujieleza, uhuru wa taasisi mbalimbali za watetezi wa haki za binadamu, sheria zimetungwa kali na kufanya haki za binadamu zizorote.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!