Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ateta na bosi wa BADEA
Habari za Siasa

Rais Samia ateta na bosi wa BADEA

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Uchumi Afrika (BADEA), Dk. Sidi Ould Tah. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Jumanne, tarehe 5 Oktoba 2021, Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Ould Tah amemshukuru Rais Samia kwa kuzungumza nae na kumhakikishia kuwa BADEA itaendelea kuunga mkono jitahada za Serikali ya Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Aidha, Dk. Ould Tah ameutambulisha mkakati mpya wa BADEA 2030 ambao unaainisha fursa zitokanazo na ongezeko la mtaji kutoka kwa wanahisa wake na kuwezesha kuongezeka kwa utoaji wa misaada na mikopo kwa mwaka.

Dk. Ould Tah amesema mkakati huo unajikita kwenye miundombinu, vijana na wafanyabishara wadogo na wa kati, kuongeza mnyororo wa thamani katika kilimo, biashara na sekta binafsi pamoja na kuwajengea uwezo wahusika wa miradi hiyo.

Kwa upande wake, Rais Samia ameishukuru BADEA kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika miradi ya maendeleo na utaalamu kwa zaidi ya miaka 40.

Aidha, Rais Samia ameishukuru BADEA kwa kuonyesha fursa zilizopo katika mkakati wao mpya unaoendana na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III), unaolenga kuongeza ufanisi na ushindani kwa kuimarisha miundombinu, biashara, sekta binafsi pamoja na kuwajengea uwezo vijana na wafanyabishara wadogo na wa kati.

Taarifa hiyo imetolewa na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!