Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DED anayetuhumiwa kuiba mabati 1,000 asimamishwa, Waziri Ummy asema…
Habari za Siasa

DED anayetuhumiwa kuiba mabati 1,000 asimamishwa, Waziri Ummy asema…

Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo (DED), Mkoa wa Morogoro, Asajile Mwambambe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Mwambambe anatakiwa kurudi Halmashauri ya Kilosa mkoani humo ili kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo upotevu wa mabati 1,172.

Wakati upotevu huo unatokea, Mwambambe alikuwa mkurugenzi wa Kilosa kabla ya baadaye kuhamishiwa Gairo na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Tarehe 24 Agosti 2021, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu aliwaeleza waandishi wa habari kwamba linamshikilia Mwambambale na wenzake sita kwa tuhuma ya wizi wa mabati 1,172 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 31.

Alisema taarifa zinaonesha fedha hizo zilitolewa na halmashauri ya Kilosa, kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi ya kijiji cha Mbumi kata ya Mbumi, lakini badala yake zilirudishwa kwa mbinu za ujanjaujanja.

Kamanda Musilimu alisema Juni 17 mwaka huu, kuliripotiwa tukio la wizi wa mabati yaliyohifadhiwa kwenye ghala la halmashauri ya Kilosa, na baada ya uchunguzi ilibainika hakukuwa na viashiria vyovyote vya kuvunjwa kufuli kwenye ghala hilo wala milango kubomolewa.

Leo Ijumaa, tarehe 10 Septemba 2021, Nteghenjwa Hoseah, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Tamisemi amesema, Waziri Mwalimu amemsimamisha kazi Mwambambwe ili arudi Kilosa kujibu tuhuma hizo.

Taarifa hiyo imesema, mabati hayo yamkwisha kupatikana na kurejeshwa eneo husika kuendelea na kazi iliyokuwa imekusudiwa.

Katika taarifa hiyo, imemnukuu Waziri Umma akiwataka watumishi wa wote wa umma kufanya kazi kwa weledi, kuwa waadilifu na makini katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!